Diamond Platnumz, Zuchu, Nandy Alikiba, Darassa, Harmonize na Rayvanny Watajwa Kuwania Tuzo Za AFRIMA 2021

[Picha: CitiMuzik]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Waandaaji za tuzo kubwa za muziki barani Afrika, AFRIMA hatimaye wametoa orodha ya wasanii waliochaguliwa kuwania tuzo hizo kwa mwaka huu wa 2021.

Habari njema ni kuwa kutokea nchini Tanzania wasanii mbalimbali wameteuliwa kuwania tuzo hizo akiongozwa na Diamond Platnumz ambaye ametajwa kwenye vipengele sita.

Soma Pia: Diamond Platnumz, Zuchu, Lavalava, Mbosso Wamkaribisha Msanii Mpya Wa Rayvanny Mac Voice

Diamond ametajwa kuwania tuzo ya msanii bora wa kiume Afrika mashariki, Wimbo bora wa mwaka kupitia ‘Waah’, Video bora ya mwaka ‘Waah’, Wimbo bora wa collaboration ‘Waah’, na msanii bora wa mwaka kipengele ambacho anawania pamoja na Wizkid, Davido pamoja na Burnaboy.

Mwanamuziki Zuchu amewekwa kuwania tuzo ya msanii bora wa kike wa Afrika Mashariki kipengele ambacho kinamkutanisha na Nandy, Rosa Ree na tems kutokea Nigeria.

Rapa wa kike anayefanya vizuri sana Tanzania Rosa Ree nae amepata vipengele vitatu kwenye tuzo hizo kama msanii bora wa kike Afrika Mashariki, Msanii bora wa muziki wa Reggae na Dancehall pamoja na msanii bora wa Hip-hop barani Afrika.

Soma Pia: Bongo Flava Takeover: Factors Contributing to Success of Bongo Music in Kenya

Alikiba, Darassa, Harmonize na Diamond Platnumz wote walikutanishwa kwenye kipengele cha msanii bora kiume Afrika mashariki na kwa upande wa Alikiba, unamkuta pia kwenye kipengele cha msanii anayekubalika zaidi na mashabiki.

Mastaa wengine watanzania walioshirikishwa kwenye tuzo hizo ni pamoja na Lizer Classic, Director Kenny kama mtayarishaji wa video bora wa mwaka pamoja na DJ Sinyorita ambaye ametajwa kuwania DJ Bora kutokea Afrika. Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu.

Leave your comment