Diamond Platnumz, Zuchu, Lavalava, Mbosso Wamkaribisha Msanii Mpya Wa Rayvanny Mac Voice

[Picha: Instagram ]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Habari kubwa nchini Tanzania kwa sasa ni msanii mpya wa Rayvanny Mac Voice ambaye ametangazwa kama mwanamuziki wa kwanza wa lebo ya Next Level Music siku chache zilizopita. Msanii huyo anatarajiwa kutambulishwa rasmi tarehe 24/9/2021 na zikiwa zimebaki takriban siku mbili kufikia tarehe hiyo tayari wasanii tofauti tofauti wameoneaha kumuunga mkono msanii huyo. Diamond Platnumz kupitia akaunti yake ya Instagram alichapisha picha ya msanii huyo na kuandika "The Movie Is About To Start" akimaanisha kuwa muda sio mrefu msanii huyo ataingia sokoni huku akimtag Mac Voice, Rayvanny pamoja na Next Level Music kwenye chapisho hilo

Soma pia: Jux Aachia kanda ya wimbo wake "Sina Neno"

Chapisho hili la Diamond Platnumz kwenye akaunti yake ya Instagram inaonesha kuwa Bosi huyo wa WCB amempokea msanii huyo kwa mikono miwili pamoja na kwamba ni msanii wa Rayvanny. Zuchu nae hakuwa nyuma kuonesha mchango wake kwa Mac Voice baada ya msanii huyo kuchapisha picha ya msanii huyo na kuandika "Welcome to the familiy Mac Voice" kisha kuandika tarehe ambayo msanii huyo anatarajiwa kutambulishwa rasmi. 

Baba Levo ambaye ni mtu wa karibu kwenye lebo ya WCB na mtangazaji wa Wasafi FM hakufanya ajizi kuonesha upendo alionao kwa msanii huyo baada ya kuandika kupitia akaunti yake ya Instagram : "Tarehe 24 Rayvanny anaachia mawe mapya kutoka kwa first born wake Mac Voice Tz" 

Mtunzi wa ngoma ya "Baikoko" Mbosso Khan nae alitumia muda wake kumkaribisha msanii huyo kwenye muziki baada ya kuandika "Welcome To The Winning Team Mac Voice" kwenye akaunti yake ya Instagram. 

Watu wengine mashuhuri waliomtakia heri msanii huyo ni pamoja na Kajala, Young D, Queen Darling, Don Fumbwe pamoja na Lavalava

 

Leave your comment