Jux Aachia kanda ya wimbo wake "Sina Neno"

[Picha: Jux Instagram ]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Fundi wa muziki wa Rnb kutokea Tanzania Jux hatimaye ameachia video ya ngoma yake ya "Sina Neno" Video ya "Sina Neno" inakuja takriban siku 14 tangu Jux aachie audio ya ngoma hiyo ambayo imetayarishwa na Bob Manecky na video ya wimbo huo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa muziki nchini Tanzania Video ya "Sina Neno" imeakisi moja kwa moja ujumbe uliopo kwenye wimbo na kwa ujumla ni video ta kitofauti kwani imehusisha watu watatu tu. 

Soma Pia: Rayvanny Amtambulisha Msanii wa Kwanza wa Next Level Music

Jux anaonekana akiwa ufukweni amekaa juu ya kinanda akiwa anaimba kwa hisia sana huku nyuma yake jua linaonekana likiwa linazama. Video inanoga zaidi pale mama mjamzito ambaye wimbo huo ni kwa ajili yake anaonekana akiwa sehemu mbalimbali akiwa anakula raha na mpenzi wake na bila kupepesa ni salama kusema kuwa kuanzia ubora wa picha, uchaguzi wa mandhari ya video pamoja na stori nzuri ya isiyochosha imefanya video hii kuwa bora sana. 

"Sina neno" imetayarishwa na Hanscana ambaye ni mojawapo kati wa watayarishaji video bora sana kwa nchini Tanzania akiwa ameshafanya kazi na wasanii kama Diamond Platnumz, Alikiba, Harmonize, Rayvanny, Vanessa Mdee, Barnaba ma wasanii wengine wemgi ndani na nje ya Tanzania. Kwa mwaka huu ukiweka kando na "Sina Neno" Jux ameachia ngoma mbalimbali kama "Mapepe", "Sawa" pamoja na kushirikishwa kwenye ngoma ya "My Life" ya rapa Moni Centrozone.

https://www.youtube.com/watch?v=cDxZrTIcKLk

 

Leave your comment