Tommy Flavour Athibitisha Ommy Dimpoz Kuwepo Kwenye Album Yake Mpya

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii kutokea Kings Music Tommy Flavour amethibitisha rasmi kuwa tayari ameshafanya collabo na msanii Ommy Dimpoz na ngoma hiyo inatarajiwa kuwepo kwenye albamu yake mpya.

Kwa muda mrefu sasa, Tommy Flavor amekuwa akionekana kuwa na ukaribu mkubwa na Dimpoz na hata ngoma ya Ommy Dimpoz ya kuitwa ‘Ni Wewe’, iliyotoka miaka miwili nyuma Tommy Flavour alihusika katika uandishi.

Soma Pia:  Best Naso Aachia Albamu Yenye Nyimbo 32, Afunguka Kuhusu Changamoto Alizokumbana Nazo

Kuhusu collabo yake na Ommy Dimpoz, akiwa anajibu swali aliloulizwa na Lil Ommy, Tommy Flavour alisema kwa ufupi kuwa "Ngoma ipo tayari, ipo kwenye albamu na itakuwepo.”

Kwa muda mrefu sasa, Tommy Flavour amekuwa akifanya collabo na wasanii wa Kings Music pekee, ila kwenye mahojiano hayo alidokeza kuwa albamu yake itahusisha pia wasanii nje ya Kings na Tanzania.

"Kazi zipo tayari na katika hizi back to back mojawapo ya kazi ambazo ntaziachia ndo hizo ambazo ntakuwa na wasanii wengine ambao wako nje ya Kings Music na wengine wa nje ya Tanzania," alidokeza Tommy Flavor.

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa na Mac Voice, Cheed, Barnaba na Wasanii Wengine Bongo Wiki Hii

‘Heir To The Throne’ ni albamu ya kwanza ya msanii Tommy Flavor na inatarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni mara baada ya bosi wa lebo ya Kings Music kuachia albamu yake ya ‘Only One King’ mwezi huu.

Kabla ya kuachia ngoma ya ‘Jah Jah’, Tommy Flavour aliachia remix ya ngoma ya Wizkid ‘Essence’, na kupitia mahojiano hayo, Tommy alisema kuwa aliamua kufanya remix ya ngoma hiyo ili kuwaandaa mashabiki zake na kufungua ukurasa rasmi wa muziki wake.

Leave your comment