Best Naso Aachia Albamu Yenye Nyimbo 32, Afunguka Kuhusu Changamoto Alizokumbana Nazo

[Picha: Best Naso Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii maarufu nchini Tanzania Best Naso aliachia albamu yake ya tatu wikendi hii iliyopita. Albamu hii ina jumla ya nyimbo 32 ambazo zinazungumzia mada tofauti na pia kuwahusisha wasanii kutoka sehemu mbali mbali ya bara la Afrika.

Kwa mujibu wa Best Naso, aliweka ngoma mingi sana kwenye albamu yake ili awepe mashabiki ladha tofauti ya muziki.

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa na Mac Voice, Cheed, Barnaba na Wasanii Wengine Bongo Wiki Hii

Aliongeza kuwa albamu ikiwa na nyimbo mingi basi shabiki hawezikuchoka, kwani akifikia ngoma ya mwisho atarudi mwanzo na kuisikiliza ya kwanza.

Best Naso alifichua kuwa kwenye albamu hiyo, amewashirikisha wasanii tofauti wakiwemo Aslay, Nay Wa Mitego, Gigy Money na wengine wengi.

Aidha, msanii huyo pia aliongezea kuwa alikumbwa na changamoto katika harakati ya uandilizi wa albamu yake kutokana na mfumo wake wa kuimba. Best Naso amejulikana kwa kuwa msanii wa kuhadithia katika nyimbo zake, na kama alivyoeleza ni vigumu kuwashirikisha wasanii wengine kwani msimulizi wa hadithi huwa mmoja.

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa na Mac Voice, Cheed, Barnaba na Wasanii Wengine Bongo Wiki Hii

"Nimefanya nyimbo 32 kwa sababu nimeziweka kuwa za milele, za maisha yote. Watasikiliza na hawawezi kuchoka. Utasikiliza tatu ukichoka kesho utasikiliza nyingine. Ukishasikilza 32 unajikuta umerudi tena moja unaiona mpya tena," Best Naso alisema.

"Mimi ni msanii wa story, nyimbo nyingi za story huwezi kufanya kolabo kwa sababu unasimulia. So hamuezi kusimulia watu wawili," Best Naso aliongezea.

Leave your comment