Nyimbo Mpya Zilizoachiwa na Mac Voice, Cheed, Barnaba na Wasanii Wengine Bongo Wiki Hii

[Picha: Muzik TV]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Soko la muziki nchini Tanzania limeendelea kupokea bidhaa tofauti tofauti kutoka kwa wasanii ambao wameachia ngoma ambazo zimeburudisha mashabiki. Hizi hapa ni ngoma tano kali mpya ambazo zimeachiwa na kufanya vizuri sana Tanzania wiki hii:

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa na Diamond, Rosa Ree, Beka Flavour na Wasanii Wengine Bongo Wiki Hii

Wandia – Cheed

Wiki hii Konde Gang waliadhimisha Cheed Day baada ya mwanamuziki Cheed kuachia ‘Wandia’ ambayo ni ngoma ya kwanza ya msanii huyo tangu ajiunge kwenye lebo hiyo. ‘Wandia’ ni ngoma ambayo Cheed anamwimbia mpenzi wake ambaye wanapendana sana pamoja na kupitia maisha duni. Kufikia sasa, ngoma hii imeshatazamwa mara laki mbili kumi na nane.

https://www.youtube.com/watch?v=6qWuiqyfp9E

Nenda - Mac Voice

Kutoka kwenye EP yake ya ‘My Voice’, Mac Voice ameachia rasmi ‘Nenda’ kama ngoma ya kwanza ya kwenye EP yake. Video ya ‘Nenda’ imeachiwa siku tano zilizopita na bila shaka ni video ambayo itagusa na kukonga hisia kutokana na uhalisia wake. Kufikia sasa, imeshatazamwa mara laki mbili arobaini na nane kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=N5KLB5oxcZA

Yalaaniwe Mapenzi - Barnaba

Barnaba aliachia ngoma yake ya ‘Yalaaniwe Mapenzi’ ambayo ni mpya kabisa. Kwenye ngoma hii, Barnaba analalamika jinsi ambavyo alikuwa anajitoa kwa mpenzi ila mwisho wa siku akaumizwa.

https://www.youtube.com/watch?v=d_o5YRP-G0k

Nimeachika - Amber Lulu

Mara nyingi sana watu husononeka pale wanapoachika, lakini haipo hivyo kwa mwanadada Amber Lulu ambaye anafurahi kumalizana na mahusiano aliyokuwa nayo.

https://www.youtube.com/watch?v=QuraQkvtMyc

Yeye - Linah

Linah amerudi tena kwenye Bongo Fleva na ngoma yake ya ‘Kama Yeye’ ambayo humu ndani anamsifia mpenzi wake kwa namna ambavyo anamkosha. Ngoma hii ni ishara kuwa Linah amerudi rasmi kwenye muziki.

https://www.youtube.com/watch?v=ySVSUMb9J4o

Leave your comment