Nyimbo Mpya Zilizoachiwa na Diamond, Rosa Ree, Beka Flavour na Wasanii Wengine Bongo Wiki Hii

[Picha: CloudsMedia TZ]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Jumatatu ya mwisho ya mwezi Septemba imeshawadia na soko la muziki nchini Tanzania limeendelea kupokea bidhaa tofauti tofauti kutoka kwa wasanii ambao wameachia ngoma ambazo zimeburudisha mashabiki. Hizi hapa ni ngoma tano kali mpya ambazo zimeachiwa na kufanya vizuri sana Tanzania wiki hii:

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mac Voice Aachia EP Mpya ‘My Voice’ Chini ya Next Level Music

Jah Jah - Tommy Flavour ft Alikiba

Siku chache zilizopita Tanzania yote ilizima baada ya nyota kutokea Kings music Tommy Flavour kuachia ngoma yake ya ‘Jah Jah’ aliyomshirikisha Alikiba.  Kwenye ngoma hii, Tommy anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa mambo makubwa aliyomtendea kwenye maisha yake.

https://www.youtube.com/watch?v=IM0Rs05yiSw

Samia Suluhu - Diamond Platnumz

Baada ya kutamba na ‘Naanzaje’, kwa mara nyingine Diamond Platnumz anaungana na mtayarishaji wa muziki Lizer Classic kwenye ngoma ‘Samia Suluhu’. Ndani ya dakika tatu na sekunde 46, Diamond Platnumz anampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayofanya kuwahudumia watanzania tangu aingie madarakani. Kufikia sasa, ngoma hii imeshatazamwa mara laki tatu themanini na sita kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=yONuS8TB13M

Watatubu - Rosa Ree

Muda mfupi baada ya kutangazwa kuwania tuzo ya Afrima kama msanii bora wa kike Afrika Mashariki, Rosa Ree aliamua kutikisa tena tasnia ya Hip-hop na wimbo wake wa ‘Watatubu’. Rosa Ree anatumia mdundo mkali kutoka kwa mtayarishaji wa muziki Ibra Jacko kuwakumbusha watanzania ubora wake kwenye muziki Hiphop.

https://www.youtube.com/watch?v=mti56EZufDk

Mariana - Christian Bella & CBO Music

Baada ya kutupumzisha kwa takribani miezi nane bila kutoa ngoma, hatimaye Christian Bella amerudi tena kupindua meza za muziki wa Bongo baada ya kuachia ‘Mariana’ akiwa na washiriki wa lebo yake ya CBO Music. Kwenye ngoma hii Bella na CBO wanamsifia mwanamke anayeitwa Mariana juu ya uzuri na urembo alionao na kuonesha ni kwa namna gani wanavutiwa na mrembo huyo.

https://www.youtube.com/watch?v=vhnzOKS2l5k

My Voice - Mac Voice (EP)

Siku ya ijumaa kiwanda cha Bongo Fleva kilimpokea rasmi Mac Voice msanii mpya kutokea Next Level Music ambaye aliileta kwetu EP yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘My Voice’.

‘My Voice’ imesheheni ngoma 6 ambazo ni ‘Nenda’, ‘Mama Mwenye Nyumba’, ‘Nampenda’, ‘Tamu’ ft Rayvanny, ‘Bora Peke Yangu’ ft Rayvanny pamoja na ‘Pombe’ ft Leon Lee & Rayvanny.

https://www.youtube.com/watch?v=buz4tC46WH0

Leave your comment