Nyimbo Mpya: Mac Voice Aachia EP Mpya ‘My Voice’ Chini ya Next Level Music

[Picha: Mac Voice Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii chipukizi Mac Voice ameachia EP yake ya kwanza chini ya lebo ya Next Level Music yenye jina ‘My  Voice’.

Mac Voice ndiye msanii wa kwanza kusainiwa chini ya lebo hiyo inayomilikiwa na Rayvanny. EP ya Mac Voice iliambatana na utambulisho wake. 

Soma Pia: Belle 9 Aweka Wazi Msimamo Wake Kuhusu Kujiunga na Wasafi, Konde Gang au Kings Music

EP hiyo iliyopewa jina la My Voice iko na nyimbo sita, nazo ni; Nenda, Mama Mwenye Nyumba, Nampenda, Tamu, Bora Pekee Yangu na Pombe.

Mac Voice kwenye EP hiyo amefanya kazi na watayarishaji wa miziki tofauti. Baadhi ya watayarishaji wa miziki waliohusika kwenye utengenezaji wa 'My Voice' ni Lizer Classic, S2kizzy, Sound Boy, Nuzder na Trone.

EP hiyo pia iko na kolabo kadhaa ambazo ni Tamu akimshirikisha Rayvanny, Pombe akimshirikisha Rayvanny na Leon Lee, na Bora Pekee Yangu akimshirikisha Rayvanny.

Soma Pia: Rayvanny ‘Wanaweweseka’, Jux ‘Sina Neno’ na Nyimbo Zingine Zinazotamba Bongo

Nyimbo zilizo kwenye EP hiyo zimepokelewa vizuri na mashabiki. Rayvanny kupitia ukurasa wake wa Instagram aliwashukuru mashabiki kwa kumuunga mkono na kumwonyesha upendo Mac Voice.

Aidha, Rayvanny alijilinganisha na Mac Voice kwa kusema kuwa alikuwa ameiga mfano wake.

 "Like father like son niwashukuru wote mnao msapoti kijana wenu @macvoice_tz," chapisho la Rayvanny mtandaoni lilisomeka.

Mac Voice alikuwa amesubiriwa kwa hamu sana na mashabiki kwani utambulisho wake ulichukua muda mrefu kabla kufanyika. Rayvanny hapo awali alikuwa amesema kuwa hana pupa ya kumtoa msanii, na alikua anafuata mikakati na taratibu zilizoekwa na lebo usimamizi wa Next Level Music.

https://www.youtube.com/watch?v=buz4tC46WH0

Leave your comment