Belle 9 Aweka Wazi Msimamo Wake Kuhusu Kujiunga na Wasafi, Konde Gang au Kings Music

[Picha: GetMziki]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki mwenye heshima yake kwenye muziki wa Bongo Fleva Belle 9 hivi karibuni ameweka wazi msimamo wake, iwapo atapata ofa ya kujiunga na lebo kubwa tatu kubwa nchini Tanzania yaani Wasafi ya Diamond Platnumz , Konde Gang ya Harmonize au King's Music ya Alikiba.

Akiongea kwenye kituo kimoja cha redio hapa Tanzania, Belle 9 alisema kuwa iwapo atapata ofa ya kujiunga na mojawapo kati ya lebo hizo, basi yeye yuko tayari kwani kikubwa ni kufanya biashara.

Soma Pia: Harmonize Ahairisha Utambulisho wa Cheed Huku Rayvanny Akimpigia Mac Voice Kampeni

"Mimi niko tayari kufanya kazi na record label yoyote kufanya kazi na management yoyote. Mimi ni mfanya biashara," alizungumza Belle 9.

Belle 9 aliongeza kuwa yeye linapokuja suala la kazi hachagui upande wowote wa kufanya nao kazi.

"Sina side maalum kwamba watu flani wakinihitaji ndo ndo ntakubali. Watu flani wakinihitaji labda ntakataa mimi sina side maalum ikitokea mtu yeyote anataka tufanye kazi tunafanya kazi," alisema Belle 9.

Soma Pia: Rayvanny ‘Wanaweweseka’, Jux ‘Sina Neno’ na Nyimbo Zingine Zinazotamba Bongo

Kauli hii ya Belle 9 inashabiana vyema kabisa na kauli ya Jay Melody aliyoitoa siku kadhaa nyuma akiwa kwenye mahojiano na Lil Ommy kuwa yuko tayari kujiunga na lebo yoyote ya muziki hapa nchini Tanzania ili mradi tu kutakuwa na maelewano mazuri kati ya pande hizo mbili.

Kwa sasa , Belle 9 anatamba na wimbo wake wa ‘Wekaweka’ ambao umeandaliwa na mtayarishaji wa muziki Vennt Skillz kutokea kwanza records.

Leave your comment