Tommy Flavour Apinga Vikali Mahusiano Katili

[Picha: Afro Hits]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii maarufu wa muziki wa bongo Tommy Flavour amejitokeza na kupinga vikali mahusiano katili. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Tommy ambaye amesainiwa katika lebo ya King's Music aliwashauri wafuasi wake kuepuka mauhusiano hayo. Tommy Flavour alieleza kwa upana maana ya mahusiano katili na aina zake.

Kwa mujibu wa msanii huyo, haya mahusiano yanawezakuwa ya kimapenzi, kikazi, kirafiki au kifamilia. Aliendelea kwa kutoa mifano ya hali ambazo zinawezasababisha mahusiano katili.

Soma Pia: Harmonize Adokeza Nia ya Kufanya Collabo na Tunda Man

Baadhi ya hali hizo ni pamoja na; ukosefu wa heshima, unyanyasaji na ukatili wa kiakili/kisaikolojia au kimwili, usaliti, ugomvi na kukosekana kwa upendo wa dhati.

Tommy Flavour alifichua kuwa yeye binafsi amewahi kujipata katika mahusiano katili, ila kwa bahati nzuri alijitoa mapema.

"Mimi (Tommy Flavour) ni Mhanga wa mahusiano ya namna hii, na nitashare nanyi story hiyo leo, lakini la msingi nilifanikiwa kujiondoa kwenye na kupata sehemu nyingine niliyopata thamani yangu, heshima na upendo," Tommy Flavour aliendaka mtandoani.

 "Je wewe upo au uliwahi kuwa kwenye mahusiano katili? Share nami your story kuhusu mahusiano yako. Tuungane kuvunja ukimya na ku share stories zetu, huwezi kujua utamsaidia nani kupitia story yako au unaweza kupata msaada zaidi kupitia hapa na ukatibu majeraha ya mahusiano katili," ujumbe wa msanii huyo uliendelea.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny ft. Zuchu ‘I Miss You’ na Ngoma Zingine Mpya Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii

Tommy Flavour, hata hivyo, hakufichua iwapo kuna kisa kilichompa motisha ya kuchapisha ujumbe huo.

Leave your comment