Harmonize Adokeza Nia ya Kufanya Collabo na Tunda Man

[Picha: Habari Leo]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Bosi wa lebo ya Konde Music Worldwide Harmonize amefunguka namna ambavyo anatamani kufanya collabo na msanii mkongwe kutokea Tanzania Tunda Man, ambaye ni muasisi wa lebo ya Tip Top Connection.

Harmonize ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya ‘Serious Love’, kupitia akaunti yake ya Instagram alionesha kuwa Tunda Man ni msanii ambaye tangu akiwa mdogo alikuwa anaimba na kutumbuiza ngoma zake na alikuwa akimkubali sana kiasi cha kujiita Tunda Man.

Soma Pia: Otile Brown, Harmonize Wajipiga Kifua Kuhusu Ujio wa Kolabo Yao

"Legend Tunda Man ft Kondeboy dunia inakimbia sanaa I just remember when I used to call my self Tundaman & singing his music in da primary school some une tell my brother I love it recording tonight," aliandika Harmonize kwenye Instastory.

Huu ni muendelezo wa msanii Harmonize kuonesha upendo alionao kwa wasanii wakongwe kwani mwezi Oktoba mkali huyo wa Swahili Amapiano kupitia Instastory alitangaza kufanya collabo na Twenty Percent mara tu atakapotua nchini Tanzania kutoka Marekani, collabo ambayo kufikia sasa bado haijatoka.

Soma Pia: Harmonize Afichua Mpango Wake wa Kuachia Ngoma 12 Mwaka wa 2022

Wasanii wengine wakongwe ambao Harmonize tayari ameshafanya nao kazi ni pamoja na Dully Sykes ambaye amefanya nae ngoma tatu ambazo ni ‘Inde’, ‘Kadamshi’ na ‘Nikomeshe’.

Kando na Dully Sykes, mkongwe mwingine ambaye Harmonize amefanya nae ngoma ni pamoja Q Chillah ambaye pia amefanya nae ngoma tatu ambazo ni ‘Go Low’, ‘My Boo Remix’ pamoja na ‘Nionyeshe’ ambayo ilifanya vizuri mno.

Leave your comment