Otile Brown, Harmonize Wajipiga Kifua Kuhusu Ujio wa Kolabo Yao

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wasanii nyota kutoka Afrika Mashariki Harmonize na Otile Brown wamejipiga kifua kuhusu ujio wa kolabo yao. Harmonize kupitia ukurasa wake wa kijamii alidai kuwa mchango wake kwenye kolabo hiyo wafaa kumpa heshima kubwa kutoka kwa mashabiki wake walioko Kenya.

Alisema kuwa ametenda haki kwenye ngoma hiyo aliyoshirikishwa na msanii wa Kenya Otile Brown.

Soma Pia: Harmonize Afichua Mpango Wake wa Kuachia Ngoma 12 Mwaka wa 2022

"Please everybody especially Kenyans put some respect on me for how I murdered Otile Brown song," ujumbe wa Harmonize kwenye ukurasa wake wa Instagram ulisomeka.

Otile Brown kwa upande wake alikubali kuwa Harmonize alikuwa amefanya kazi nzuri kwenye wimbo huo. Aliongeza kuwa yeye mwenye hajawaangusha mashabiki wake kwani aliyoyafanya kwenye ngoma hiyo pia sio madogo.

Aidha, Otile Brown alifichua kuwa anasubiri kumaliza mazishi ya bibiye aliyeaga hivi karibuni kabla ya kuendelea na utengenezaji wa ngoma hiyo.

Soma Pia: Ujumbe Wa Harmonize Kwa Country Wizzy Baada Ya Mkataba Wake Na Konde Gang Kukamilika

 "Yeah, he did kill his verse, and y'all know Obizee doesn't disappoint, laying Grandma to rest this weekend then we stepping on necks," Otile Brown aliandika.

Hapo awali wawili hao walitangaza kuwa watatengeneza EP itakayojumuisha nyimbo zao. Hawajafichua iwapo ngoma waliyokuwa wakizungumzia itakuwemo kwenye EP hiyo au itakuwa ngoma huru.

Harmonize alikutana na Otile Brown alipokuwa nchini Kenya kwa ziara yake ya muziki. Wawili hao ni mastaa wa muziki wa bongo si Afrika Mashariki tu bali barani Afrika.

Leave your comment