Ujumbe Wa Harmonize Kwa Country Wizzy Baada Ya Mkataba Wake Na Konde Gang Kukamilika

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Bosi wa lebo ya Konde Music Worldwide Harmonize amemuaga rasmi msanii Country Wizzy baada ya mkataba wake na lebo hiyo kukamilika. Kupitia chapisho aliloliweka kwenye ukurasa wake wa kijamii, Harmonize alionyesha upendo kwa Country Wizzy.

Nyota huyo wa muziki wa bongo vile vile alimshukuru Country Wizzy kwa mchango wake kwenye lebo ya Konde Music. Alimtakia mema rapa huyo ambaye hivi karibuni alikaribishwa kwenye lebo ya Roof Top.

Soma Pia:  Lebo Tano Kutoka Tanzania Zinazotarajiwa Kufanya Vizuri Mwaka 2022

Harmonize alikamilisha ujumbe wake kwa kumuambia Country Wizzy kuwa atamuunga mkono kwenye taaluma yake ya muziki. "Thank you fo representing big gang 2 years love you bro and I wish you all the best go make me proud always got your back go and shine rasta," ujumbe wa Harmonize ulisomeka.

Kando na ujumbe huo, Harmonize aliweka sherehe ya kumuaga Country Wizzy nyumbani kwake. Sherehe hiyo ilihudhuriwa na wadau tofauti ikiwemo rapa Young Lunya ambaye ako na ukaribu mno na msanii Country Wizzy.

Soma pia: Mabantu Wafunguka Jinsi Walivyompata Harmonize Kwenye "Utamu Remix"

Country Wizzy anaonekana kuondoka katika lebo ya Konde Music Worldwide kwa amani, tofauti na tetesi zilizoko mtandaoni kuwa huenda kuliibuka uhasama baina yake na usimamizi wa lebo hiyo.

Country Wizzy, hata hivyo, amebaki kimya kuhusu kuondoka kwake lebo ya Konde Music Worldwide. Kufikia sasa hajatoa taarifa yoyote pia kuhusu usimamizi wake mpya.

 

Leave your comment