Mabantu Wafunguka Jinsi Walivyompata Harmonize Kwenye "Utamu Remix"

[Picha: Mabantu Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

"Utamu Remix" ya kwao Mabantu wakimshirikisha Harmonize ni moja ya ngoma inayofanya vizuri sana kwa sasa nchini Tanzania na hivi karibuni Muuh Mabantu ambaye ni mshiriki wa kundi hilo la Mabantu alfunguka mchakato waliopitia, mpaka Harmonize kushiriki kwenye remix ya ngoma hiyo.

Soma Pia: Diamond Platinumz Adokeza Ujio Mpya Wa Queen Darleen

Akizungumza kwenye kipindi cha Zege cha Times FM Muuh Mabantu alifichua kuwa baada ya kuachia ngoma hiyo, bila ya kutarajia meneja wa msanii Harmonize Choppa aliwapigia simu na kukiri kuwa Harmonize ameipenda sana ngoma yao ya "Utamu" na hivyo meneja akaomba wafanye remix ya ngoma hiyo.

"Nakumbuka mara ya kwanza kupokea simu ilikuwa ni simu ya Meneja Choppa alitupigia simu anahitaji kukutana na sisi. Baada ya kukutana na sisi tukaweza kukamilisha hili suala na Bro (Harmonize) alituambia kuwa Utamu ndo nyimbo pendwa sana kwake ambayo amekuwa akiisikiliza muda wote" alizungumza Muuh Mabantu.

Aidha kupitia mahojiano hayo Muuh Mabantu alimshukuru sana Harmonize kwa kushiriki kwenye ngoma hiyo ya "Utamu Remix" na kumpongeza Harmonize kwa kuweza kuupeleka mbele muziki wa Tanzania.

"Harmonize ni brother ambaye ametutanguliavitu vingi kiukweli especially kwenye muziki na pia unapozungumzia wasanii ambao wanatuwakilisha nchi yetu kwenye mataifa mengine huwezi kuacha kukosa kumtaja Harmonize" alizungumza mshiriki huyo wa kundi la Mabantu Tangu iingie sokoni.

"Utamu Remix" imekuwa ni ngoma pendwa sana kwa watanzania, na kufikia sasa imeshatazamwa mara laki tisa kumi na sita ndani ya wiki nne tu.

https://www.youtube.com/watch?v=gZErfeebky0

Leave your comment