Harmonize Afichua Mpango Wake wa Kuachia Ngoma 12 Mwaka wa 2022

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki wa bongo Harmonize ametangaza kuwa mwaka huu ataachia nyimbo kumi na mbili.

Harmonize aliweka tangazo hilo wazi kupitia ukurasa wake wa Instagram. Kwenye chapisho hilo, Harmonize vile vile alifichua kuwa nyimbo hizo kumi na mbili zipo tayari na kilichosalia ni kuziachia tu.

Soma Pia: Nyimbo za Beka Flavour ‘Libebe’ na ‘Sikinai’ Zafutwa YouTube

Bosi huyo wa Konde Music Worldwide amesema atakuwa akiachia wimbo moja kila mwezi hadi mwaka uishe. Aliendelea kwa kusema kuwa wimbo wa kwanza kati ya hizo kumi na mbili itatoka mwezi huu wa Januari.

Alisisitiza kuwa ngoma hiyo ya kwanza itatikisa tasnia ya muziki wa Tanzania.

"Usidhani High School inatosha. Nina nyimbo 12 tayari na kila mwezi naachia nyimbo moja. Hii january nitaachia wimbo ambao utachezwa kwenye kila matamasha na dini zote," Chapisho la Harmonize mtandaoni lilisomeka.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Platform TZ Aachia Ngoma Mpya ‘Who’

Harmonize anaonekana kuendelea kuongeza uzito wa jina lake kwenye muziki kwa kuzidisha bidii na kuachia ngoma mingi.

Konde Boy, kama anavyofahamika kimuziki, vile vile anaendelea kuachia video za nyimbo zilizoko kwenye albamu yake ya 'High School'. Albamu hiyo ambayo ilikuwa ya pili kutoka kwa msanii huyo ilipata mapokezi mazuri miongoni mwa mashabiki.

Kufikia sasa, Harmonize ameachia video ya ngoma mbili kutoka kwenye albamu hiyo. Video ya kwanza kuachiwa ilikuwa ya wimbo wa 'Outside' huku wimbo wa pili ukiwa wa 'Serious Love'

Leave your comment