Nyimbo Mpya: Platform TZ Aachia Ngoma Mpya ‘Who’

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki anayekuja kwa kasi kwenye kiwanda cha Bongo Fleva Platform ameachia ngoma mpya kabisa ya kuitwa ‘Who’.

 Ngoma hii ya ‘Who’ kutoka kwa Platform ni ngoma ya kwanza ya msanii huyo kwa mwaka huu wa 2022. ‘Who’ ni ngoma inayokuja wiki tatu tangu aachie ‘Vitamu’ ambayo alifanya na Ruby.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Diamond ‘Unachezaje’, Harmonize ‘Serious Love’ na Ngoma Zingine Zinazotamba Tanzania Wiki Hii

‘Who’ ni ngoma ambayo imebeba ujumbe mzito wa mapenzi. Ndani yake Platform anaonesha ni jinsi gani ambavyo anaumizwa na mapenzi kwani mtu aliyempenda sio mwaminifu kwenye mahusiano.

Ukisikiliza ngoma hii, pengine yaweza kukumbusha ngoma ya ‘Asante’ ya kwake Marioo au hata ngoma ya ‘Mhudumu’ ya kwake Aslay Isihaka.

Soma Pia: Matukio 5 ya Kimuziki Yanayotarajiwa Kutikisa Bongo Mwaka wa 2022

Kibao hiki kimetayarishwa na Mafeeling TZ mtayarishaji wa muziki ambaye kufikia sasa ameshafanya kazi na wasanii tofauti kutokea Tanzania kama Rose Ndauka, Aslay Isihaka, Kayumba pamoja na Hanstone.

Video ya ‘Who’ imetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu huku Director Beel ambaye ndiye ameelekeza kazi hii akiipamba video ya ‘Who’ kwa stori nzuri iliyojawa na uhalisia ambayo imeendana barabara na mashahiri ya ngoma hii.

Kufikia sasa, video ya ngoma hii imeshatazamwa takriban mara ishirini na sita elfu kwenye mtandao wa YouTube ikiwa ni masaa machache tangu ngoma hii iingie sokoni.

https://www.youtube.com/watch?v=vm9HWj3vYTY

Leave your comment

Top stories

More News