Nyimbo za Beka Flavour ‘Libebe’ na ‘Sikinai’ Zafutwa YouTube

[Picha: Muziki TV]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Beka Flavour amepata pigo kwenye safari yake ya kimuziki baada ya ngoma zake mbili kufutwa kwenye akaunti yake ya YouTube.

Beka Flavour ambaye alikuwa ni mshiriki wa kikundi cha Yamoto Band alitumia ukurasa wake wa Instagram kuthibitisha kuwa ni kweli ngoma zake mbili ambazo ni ‘Libebe’ pamoja ‘Sikinai’ kwa miezi takriban miwili sasa hazionekani wenye akaunti yake ya YouTube.

Soma Pia: Producer S2kizzy Aeleza Sababu ya Wasanii Wengi Watanzania Kufanya Amapiano

Kwenye chapisho hilo, Beka alieleza kuwa walijaribu kuwasiliana na Youtube ili kujua nini kimesababisha hali hiyo, na kwa mujibu wa YouTube walieleza kuwa video hizo mbili zilifutwa na moja kati ya watu wanaofanya kazi na Beka Flavour.

"Samahanini mashabiki wangu wote mmekua mkiulizia video zangu mbili ambazo hazionekani YouTube mda mrefu sana video ya #LIBEBE na #SIKINAI, ni kweli video hizo zimefutwa kwenye acount yangu ya YouTube yapata miezi miwili sasa toka zimefutwa na hatujui zimefutwa na nani japo tulijaribu kuwasiliana na YouTube wenyewe walituambia video hizo zimefutwa na mtu ambae tunafanya nae kazi so hatujajua nani ambae amezifuta video hizo.

Soma Pia: Ujumbe Wa Harmonize Kwa Country Wizzy Baada Ya Mkataba Wake Na Konde Gang Kukamilika

“Tunaendelea kupambana ziweze kurudi japo sina uhakika kama zitarudi., yote ya yote mapambana yanaendelea kazi nzuri na zenye ubora zaidi zinakuja 2022 me mnyonge bwana," ulisomeka ujumbe huo wa Beka Flavour.

Hii si mara ya kwanza kwa video ya msanii kutoka Tanzania kufutwa kwenye mtandao wa YouTube kutokana na sababu tofauti tofauti. Mwaka 2017 video ya ‘Hela’ ya msanii Madee ilifutwa Youtube na mwaka 2020 ‘Cheche’ ya kwake Zuchu na Diamond Platnumz ilipotea kwa muda Youtube kisha ikarejea. 2021 ‘Wivu’ ngoma ya Maua Sama na Aslay pia iliondolewa YouTube na kurudishwa baada ya muda.

Leave your comment