Khadija Kopa Azungumzia Uhusiano Baina ya Diamond na Zuchu

[Picha: The Star]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota wa mtindo wa taarab Khadija Kopa, ambaye pia ni mamake msanii Zuchu, kwa mara ya kwanza amezungumzia uvumi uliopo mtandaoni kuhusu uhusiano wa kimapenzi baina ya mtoto wake na Diamond Platnumz.

Tuhuma za uhusiano baina ya Zuchu na Diamond zimeibuka na kutawala mtandao kwa siku za hivi karibuni. Japo wawili hao wamebaki kimya kuhusu tuhuma hizo, mengi yamesemwa na habari hizo hatimaye zilimfikia mamake Zuchu kupita mahojiano na Wasafi TV.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Zuchu Aachia 'Mwambieni’

Kwa mujibu wa Khadija Kopa, hajapata taarifa zozote za uhusiano huo kutoka kwa Zuchu au Diamond. Alisema kuwa hakuna mahari yaliyopelekwa kwake, au utambulisho wa Diamond uliofanywa nyumbani kwake.

"Nakwambia kama angekuwa mkwe wangu mtarajiwa, angekua ashakuja nyumbani, ashatoa mahari, ningekuambia mkwe wangu mtarajiwa. Japo kuvishwa pete sio kuolewa, manake unawezavishwa pete, unaweza kuposwa lakini mtu aioe... Diamond sio mkwe wangu mtarajiwa kwa sababu hajaja kuposa wala sijasikia chochote. Kwa hiyo sio mkwe wangu mtarajiwa," Khadija Kopa alisema.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nandy Aachia Video ya ‘Party’ Akiwashirikisha Billnass na Mr Eazi

Aidha, Khadija Kopa pia alitupilia mbali tuhuma za uhusiano mbaya baina yake na Mama Dangote ambaye ni mama ya Diamond. Alisema kuwa yeye ana uhusiano mzuri na Mama Dangote na wakati mwingi wanacheka na kufurahi pamoja wanapokutana.

Khadija Kopa, vile vile, anatarajiwa kusheherekea kuitimisha miaka 30 kwenye muziki mwaka huu.

Leave your comment