Nyimbo Mpya: Zuchu Aachia 'Mwambieni’

[Picha: Free Music]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki mashuhuri kutokea Tanzania Zuchu ameachia ngoma yake mpya kabisa ya kuitwa ‘Mwambieni’.

‘Mwambieni’ ni ngoma yenye vionjo vya Afro-Pop na ndani yake Zuchu anatuma ujumbe kwa mpenzi wake wa zamani kuwa aache kumfuatilia na kumuuliziia mara kwa mara kwani yeye ameshaendelea na maisha yake.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nandy Aachia Video ya ‘Party’ Akiwashirikisha Billnass na Mr Eazi

‘Kaja omba nirudia kazirejesha salamu zamani kakumbukia ameumisi utamu kaacha kopa kalamba garasa kaishiwa masikini. Mpeni taarifa za beti mkwasa mi simkumbuki sini," anaimba Zuchu kwenye aya ya kwanza.

‘Mwambieni’ inakuja takriban mwezi mmoja tangu Zuchu aachie ngoma yake ya ‘Kitu’ huku ngoma hii pia ikiwa ni ngoma ya kwanza kwa mwaka 2021.

Ngoma hii inatarajiwa kufanya vizuri kutokana na mashahiri yake kuwa rahisi kukaririka na kuimbika. Kabla ya ngoma hii kutoka, Zuchu kwa muda mrefu sasa amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kuwajuza watu kuwa atatoa ngoma hivi karibuni.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Tommy Flavour Aachia Ngoma Mbili Mpya ‘Lay Down’ na ‘Kidogo’

Ngoma hii imetayarishwa na Mr Lg mtayarishaji wa muziki ambaye kando na kazi hii, pia ameshafanya kazi na Zuchu kwenye ‘Litawachoma’ ngoma ambayo Zuchu alifanya na Diamond Platnumz na kuweza kufanya vizuri sana.

Kufikia sasa, bado ‘Mwambieni’ haina video ila huenda malkia huyo kutoka WCB akaachia video ya ngoma hio hivi karibuni.

https://www.youtube.com/watch?v=_QIvgJ0Hu8Y

Leave your comment