Nyimbo Mpya: Nandy Aachia Video ya ‘Party’ Akiwashirikisha Billnass na Mr Eazi

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutokea Tanzania Nandy ameachia video mpya ya wimbo wake wa ‘Party’ akiwashirikisha Billnass pamoja na Mr Eazi.

Video ya ‘Party’ inakuja takriban mwezi mmoja tangu audio ya ngoma hiyo kuingia sokoni. Video hii inakuwa ni video ya muziki ya kwanza kutoka kwa Nandy tangu kuanza kwa mwaka 2022.

Soma Pia: Mkubwa Fella Athibitisha Msanii Mmoja Kuondoka Lebo ya WCB

Video ya ‘Party’ kama ambavyo ngoma ilivyo ni video ambayo imechangamka sana ikimuonesha Nandy akiwa kwenye mazingira ya klabu akiimba na kufurahi huku Billnass pamoja na Mr Eazi wakionekana kwenye mazingira ya studio ambayo yamepambwa vizuri.

Kinachovutia zaidi kwenye video hii ni mavazi ambayo wasanii hawa watatu wameyavaa. Aidha, mandhari, ubora wa picha pamoja na ubunifu mkubwa uliotumika kutengeneza video ni vitu vingine vya kupigiwa makofi.

Director Hanscana ndiye amehusika kutengeneza video hii ya ‘Party. Kando na Nandy, wasanii wengine ambao tayari Hanscana amefanya nao kazi ni pamoja na Diamond Platnumz kwenye ‘Iyo’, Zuchu kwenye ‘Nyumba Ndogo’ pamoja na Harmonize kwenye ‘Uno’.

Soma Pia: S2kizzy Atangaza Ujio Wa Albamu Yake Mwaka Huu

baada ya ‘Party’, Nandy pia anatarajiwa kuachia video ya ‘Kunjani’; ngoma ambayo alifanya na Sho Madjozi kutokea Afrika Kusini.

https://www.youtube.com/watch?v=pXeIsCY8iII

Leave your comment