S2kizzy Atangaza Ujio Wa Albamu Yake Mwaka Huu

[Picha: S2Kizzy Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mtayarishaji wa muziki mwenye heshima kubwa nchini Tanzania S2kizzy ametangaza ujio wa albamu yake baadaye mwaka huu.

Akizungumza katika mahojiano na Millard Ayo TV, S2kizzy alifichua kuwa albamu hiyo itakuwa na nyimbo kumi na tano na itawahusisha wasanii wakubwa kutoka sehemu tofauti duniani.

Soma Pia: Ujumbe Wa Harmonize Kwa Country Wizzy Baada Ya Mkataba Wake Na Konde Gang Kukamilika

Kwa mujibu wa mtayarishaji huyo wa muziki, wasanii kutoka mataifa yafuatayo wamehusika katika utengenezaji wa albamu hiyo; Tanzania, Afrika Kusini, Naijeria, Marekani, Uingereza, Zimbambwe, Ghana, India, Jameika na kadhalika.

S2kizzy, hata hivyo, alisema kuwa hana uhakika wa tarehe kamili ambayo albamu hiyo itatoka, ila mashabiki wake wawe tayari wakati wowote mwaka huu kuipokea kazi hiyo.

"Kama unawajua wasanii watatu wakubwa wa South Africa, basi wamo. Kama unawajua wasanii wakubwa wa Naijeria wamo, Tanzania unawajua wapo, Marekani wapo, UK wapo. hayo ndio mataifa yaliyoshiriki kwenye albamu yangu. Zimbambwe, yeeah. Ghana, yeah. India, yeah. Jamaica pia," S2kizzy alisema.

Soma Pia: Twenty Percent Akanusha Madai ya Kuingilia Upinzani wa Harmonize na Diamond

Alieleza kuwa amejitahidi kadri awezavyo kuchukua vionjo vya muziki kutoka mataifa mbali mbali ulimwenguni ikiwemo China. Cha kipekee kuhusu albamu hiyo ni kuwa kando na S2kizzy, itawahusisha watayarishaji wa muziki wachanga.

Mtindo wa watayarishaji wa muziki kutengeza albamu imepata umaarufu mkubwa barani Afrika. S2kizzy, vile vile, alizungumzia suala la mradi wake wa hivi karibuni wa kufanya kazi na wasanii chipukizi bila malipo. Aliwashukuru wadau tofauti katika tasnia ya muziki waliojitokeza kumuunga mkono.

Leave your comment