Twenty Percent Akanusha Madai ya Kuingilia Upinzani wa Harmonize na Diamond

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea Tanzania Twenty Percent amejitokeza hivi karibuni kupinga madai ya baadhi ya mashabiki kuwa anafaidika na bifu lililopo kati ya bosi wa WCB Diamond Platnumz na Harmonize.

Akiongea kwenye kipindi cha The Switch, Twenty Percent amekanusha madai hayo kwa kusema kuwa yeye ni kama kaka mkubwa kwa wasanii hao wawili na kwamba madai ya kuwa anatumika kuchochea bifu baina ya wasanii hao sio madai yenye tija.

Soma Pia: Harmonize Afichua Mpango Wake wa Kuachia Ngoma 12 Mwaka wa 2022

"Eti umesubiri Harmonize kakutaja taja ndo umeachia ngoma yako, jamani wakati mi naanza muziki alikuwa anafanya nini? Oooh Diamond amekupa hela ya kuandaa press conference, wapi? Ina maana kuwa mimi nimshike Diamond huku Harmonize nimwache kule. Mi ni brother wa aina gani? Kuliko kupata mmoja si bora ukose wote tu," alizungumza Twenty Percent.

Twenty Percent alizidi kuweka bayana kuhusu madai hayo kwa kusema "Hasa mimi mtu kama Harmonize au Diamond anitumie kama dongo au silaha ya kumpiga mwenzie inawezekana vipi au ngao. Yaani nyuma yangu yangu mimi we tangulia brother! Aaah mi siko hivo."

Soma Pia: Producer S2kizzy Aeleza Sababu ya Wasanii Wengi Watanzania Kufanya Amapiano

Aidha Twenty Percent ambaye alikuwa akizungumza kwa hisia sana kwenye mahojiano hayo aliweka wazi kuwa anakwazika na baadhi ya vyombo vya habari nchini Tanzania kumuuliza maswali ya mitego ambayo hupelekea watu wengi kuhisi kuwa ana upendeleo.

"Wewe ukiniuliza mimi hivi Diamond unamfikiriaje, unatarajia ntasema nini? Au ukiniuliza swali ambalo nikijibu tu Diamond ndo baba yetu, mi ntajibu swali hilo? Maana sometimes mnauliza maswali ambayo yanatutoa mpaka kwenye kile kipindi ambacho tulichonacho," alizungumza Twenty Percent.

Leave your comment