Nandy Adokeza Ujio wa Video ya ‘Kunjani’

[Picha: Premium News]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Nandy hivi karibuni ametoa taarifa kwa mashabiki zake kuwa video ya ngoma yake ya ‘Kunjani’ ipo tayari kwa ajili kuingia sokoni.

Soma Pia: Collabo 10 Kali Kutoka Tanzania Zilizofanya Vizuri Zaidi Mwaka 2021

Nandy ambaye alianza kufahamika kimuziki kupitia shindano la Tekno Own The Stage alitumia akaunti yake ya Instagram kutoa taarifa hizo kwa mashabiki zake baada ya kupakia video ambayo inamuonesha yeye na Sho Madjozi wakiwa wanashuka kutoka kwenye ndege huku ujumbe wa video hiyo uliashiria kuwa muda wowote video ya "Kunjani" inaingia sokoni.

"Hamjambo ndo tuko tayari kuwapa video," aliandika Nandy kwenye ukurasa wake wa Instagram.

 Ngoma ya ‘Kunjani’ ni ngoma ya kuchezeka yenye mahadhi ya Amapiano na ngoma hii imemuweka Nandy kwenye orodha ya wasanii wa kike Tanzania ambao wameshafanya ngoma za Amapiano.

Soma Pia: Matamasha ya Muziki Tanzania Yaliyofanya Vizuri Zaidi Mwaka 2021 

Wasanii wengine ni pamoja na Zuchu kupitia ‘Kitu’ na Mwasiti kupitia ‘Shika’; ngoma ambayo alimshirikisha Baba Levo.

‘Kunjani’ inatarajiwa kuwa video ya kwanza kutoka kwa Nandy kwa mwaka 2022 kwani miezi mitatu kabla yaani Septemba 2021 aliachia video yake ya ‘Yuda’ na kabla ya hapo mwezi Julai, aliachia video ya ngoma yake pendwa ya ‘Nimekuzoea’ ambayo kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 9.7 kwenye mtandao wa YouTube.

Leave your comment