Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Video ya 'Stay' Akimshirikisha Abby Chams

[Picha: Rayvanny Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Nyota wa muziki wa bongo Rayvanny ameachia video ya wimbo wake wa 'Stay' aliyomshirikisha msanii maarufu Abby Chams.

Ngoma ya Stay inapatikana kwenye EP ya Rayvanny iliyopewa jina la 'New Chui' iliyotoka mwaka jana.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Platform TZ Aachia Ngoma Mpya ‘Who’

'Stay' inazungumzia mapenzi ya kudumu milele. Kwenye ngoma hiyo, wahusika wanaahidiana kuwa hawataachana na watakaa pamoja daima.

Ngoma hiyo yenye kasi ya chini na mahaba tele inafunguliwa na sauti ya Rayvanny ya kumtoa nyoka pangoni.

Soma Pia: Diamond Platinumz Adokeza Ujio Mpya Wa Queen Darleen

"Looking at the sunrise Reminds me far away where we came from. That makes me realize you love me every day. When I see you home So if you are going to stay, stay forever If you are going to leave, then do it today If you are going to change, change for better If you gonna talk, make sure you mean what you say And I promise that I won't hurt you Promise that I will keep you safe. Together whatever you will be fine Girl I promise that I will love you Promise that I will care Forever and ever you will be mine, Rayvanny anafungua ngoma hiyo kabla ya Abby Chams kuingia kwenye sehemu ya pili.

Video ya ngoma hiyo imeelekezwa na Eris Mzava. EP ya New Chui inayopatikana ngoma ya 'Stay' imetayarishwa chini ya lebo ya WCB kwa ushirikiano na lebo ya Next Level Music.

https://www.youtube.com/watch?v=ZcMjitjY-GI

Leave your comment

Top stories

More News