Nyimbo Mpya: Killy Aachia Video ya 'Ni Wewe' Akimshirikisha Harmonize

[Picha: Killy Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii maarufu kutoka Tanzania Killy ameachia video ya wimbo wake wa 'Ni Wewe' aliyomshirikisha Harmonize.

'Ni Wewe' ni ngoma inayozungumzia mapenzi. Mhusika kwenye ngoma hiyo anaelezea jinsi amempenda mpenzi wake kwa dhati. Mistari ya 'Ni Wewe' inachora picha ya hali ya mapenzi yaliyonoga.

Soma Pia: Harmonize Afichua Mpango Wake wa Kuachia Ngoma 12 Mwaka wa 2022

Killy ndiye anayefungua wimbo huo kwa sauti yake nyororo kabla ya Harmonize kuingia kwenye sehemu ya pili.

"Kama mapenzi ni uchawi umeniendea ngende Maana nahisi nimezaliwa nge nikupende Aah..!! Jangwani pakavu umeota mtendee Eeh..!! Waubani waubavu sema wapi twendeee. Jua mapenzi ni siri iiiih yani toka enzi zile za mababu. Usije ukaghairi babee mazoea yakanipa tabuu uuuh. Aaaaah chuchuchu basi nipe hata kiduchu. Sifa ya mume awe na uchu usiruhusu nikapiga puchu. Eeeeeh chuchuchu basi nipe hata kiduchu. Sifa ya mume awe na uchu. usiruhusu nikapiga puchuuuuh uuuh uh. Oooh baby you make me sing this song," Killy anaimba sehemu yake ya kwanza.

Ngoma hiyo imesukwa na mtayarishaji wa muziki anayefahamika kama Hunter. Mdundo wa ngoma hii umetokana na ngoma ya kale ya 'Sina Makosa' iliyoimbwa na Les Wanyika.

Soma Pia: Otile Brown, Harmonize Wajipiga Kifua Kuhusu Ujio wa Kolabo Yao

Video kwa upande mwingine imeelekezwa na Director Ivan. Kwenye video hiyo, wahusika wamevaa mavazi ya zamani ili kuleta mandhari ya wimbo halisi wa 'Sina Makosa'.

Video ya 'Ni Wewe'imepokelewa vizuri na mashabaki na tayari ishatazamwa na maelfu ya mashabiki ndani ya muda mfupi.

https://www.youtube.com/watch?v=CRcm6EeFPNI

Leave your comment