Nyimbo Mpya: Lava Lava ‘Ng’ari Ng’ari, Chege ‘Sinsima’ na Ngoma Zingine Mpya Tanzania Wiki Hii

[Picha: Citi Muzik]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Imekuwa ni wiki ya baraka sana kwenye soko la Bongo Fleva kwani wasanii kutokea nchini Tanzania wameendeleza utamaduni wao wa kuachia ngoma kali ambazo bila shaka zimewafurahisha wafuasi wao.

Zifuatazo ni ngoma tano mpya kutoka kwa wasanii wa Tanzania kwa wiki hiii :

Soma Pia: Mbosso ‘For Your Love’, Ibraah ‘Addiction’ na Nyimbo Zingine Zinazovuma YouTube Tanzania Wiki Hii

Sinsima - Chege ft Saraphina

Baada ya ‘Kushki’ kufanya vizuri, mwanamuziki Chege ameachia ‘Sinsima’ ambayo amemshirikisha The Melanin Queen Saraphina. Kwenye ngoma hii, Chege anamsihi Saraphina afike kwenye hafla ambayo ameiandaa yeye na marafiki zake huku Saraphina nae akitumia sauti yake nzuri kumjibu Chege kuwa yuko njiani hivyo Chege asiwe na shaka.

https://www.youtube.com/watch?v=08kkM-Palv8

Paradiso Album – Stamina

Rapa Stamina wiki hii ameachia albamu yake iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa ya kuitwa ‘Paradiso’. Albamu hio imesheheni ngoma 13 za moto huku akiwa ameshirikisha wasanii kama Barakah The Prince, Aslay, Kayumba, Saraphina, Isha Mashauzi na wengineo wengi. Hii ni albamu ya pili kutoka kwa Stamina baada ya albamu yake ya ‘Mlima Uluguru’ ya mwaka 2015.

Soma Pia: ‘Sukari’ ya Zuchu Yaweka Rekodi Mpya YouTube Tanzania

Ng'aring'ari – Lava lava

Kutoka lebo ya WCB, Lava lava wiki hii alitetemesha kiwanda cha muziki Tanzania na ngoma yake ya ‘Ng'aring'ari’ ambayo ndani yake anaeleza jinsi gani amezama kwenye penzi jipya. Ngoma imetayarishwa na Lizer Classic kutokea Wasafi Records pamoja na Gopabeatz.

https://www.youtube.com/watch?v=gK5KjpqRTDE

Wa2wangu Album - Chidi Benz

Chidi Benz hatimaye aliachia albamu yake ya ‘Wa2wangu’ ambayo imesheheni ngoma 18.  Kwenye alabamu hii, amewashirikisha wasanii tofauti tofauti kama Scar Mkadinali, Only 1 Pabo pamoja na Brian Simba. Hii ni albamu yake ya pili tangu aanze muziki.

Weupe - Motra The Future

Rapa Motra The Future amerudi tena na ngoma yake mpya ya kuitwa ‘Weupe’. Kwenye ngoma hii,  rapa huyu anagusia masuala tofauti tofauti kama chuki na mikwaruzano kwenye muziki, umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii, na mambo mengine mengi. Mr T Touch ndiye amehusika katika kuandaa kazi hii.

https://www.youtube.com/watch?v=8cWj3qr3RtA

Leave your comment

Top stories