Mbosso ‘For Your Love’, Ibraah ‘Addiction’ na Nyimbo Zingine Zinazovuma YouTube Tanzania Wiki Hii

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwaka unpokaribia kuisha, wasanii wa Bongo wanazidi kuachia kazi mpya ambazo zinafanya vyema kwenye YouTube. Makala hii inaangazia ngoma tano kutokea nchini Tanzania ambazo zinavuma YouTube wiki hii.

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa na Ibraah, Nandy na Maua Sama Tanzania Wiki Hii

For Your Love - Mbosso ft Zuchu

Zimetimia wiki tatu tangu Mbosso aachie video ya ‘For Your Love’ na tangu kuachiwa kwake, ngoma hii imekuwa ni pendwa sana kwa mashabiki kutokana na ubora wa ngoma yenyewe pamoja na video. Kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 2.5 kwenye mtandao huo.

https://www.youtube.com/watch?v=3GHmlVDSRPA

Addiction - Ibraah ft Harmonize

Ngoma ya ‘Addiction’ ambayo ina vionjo vya Amapiano imeendelea kufanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube ikiwa ni ngoma ya tano kutoka kwa Ibraah kwa mwaka huu.

https://www.youtube.com/watch?v=mL3yrU792bA

Outside - Harmonize

Video ya ‘Outside’ ya kwake Harmonize imeendelea kuwika na kufanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube. Hii ni kutokana na ubora wa video yenyewe ambayo imeongozwa na muongozaji wa video za muziki kutokea nchini Nigeria wa kuitwa TG Omori.

https://www.youtube.com/watch?v=TW3lmdLTzjE

Karibuni Kibaha - Maarifa

Kazi nzuri kutoka kwa Mr T Touch ambaye alitayarisha ngoma hii pamoja na Swahili Studios ambaye alitayarisha video imefanya kazi hii kutoka kwa bingwa wa Hiphop nchini Tanzania Maarifa iwe kali sana.

https://www.youtube.com/watch?v=AT_3YvfUCtI

Bia Tamu - Marioo

‘Bia Tamu’ ya Marioo imeendelea kushikilia kwenye chati za juu kwa upande wa YouTube nchini Tanzania. Kufikia sasa video hii imeshatazamwa mara Milioni 2.4 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=J5Ka53RZUtE

Leave your comment

Top stories