Nyimbo Mpya Zilizoachiwa na Ibraah, Nandy na Maua Sama Tanzania Wiki Hii

[Picha: The Standard]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Imekuwa ni wiki nzuri sana kwenye soko la muziki nchini Tanzania kwani wasanii tofauti tofauti wameachia ngoma kali ambazo bila shaka zimezua tabasamu kwa mashabiki. Zifuatazo ni ngoma tano mpya ambazo zimeachiwa na wasanii kutokea nchini Tanzania kwa wiki hii:

Addiction - Ibraah ft Harmonize

Baada ya kufanya vizuri na ngoma yao ya ‘One Night Stand, Ibraah na Harmonize wamerudi tena na ngoma mpya ya kuitwa ‘Addiction’. ‘Kwenye ‘Addiction’, Ibraah na Harmonize wanasifia ubora wa pombe huku wakitoa tahadhari kuhusu madhara anayoweza kupata mtu iwapo atazidisha kunywa pombe.

https://www.youtube.com/watch?v=mL3yrU792bA

Safari (EP) - K2ga

Kutoka lebo ya King's Music, mwanamuziki K2ga ameachia EP yake ya kuitwa ‘Safari’ ambayo imesheheni ngoma tatu ambazo ni ‘Ni wewe’, ‘Danga’ pamoja na ‘Goma. Safari ni EP ya kwanza kutoka kwa K2ga na inategemewa kufanya vizuri sana ndani na nje ya nchi.

https://www.youtube.com/watch?v=6IPxMV2X4jA

Baba Jeni - Maua Sama

Mdundo mkali kutoka kwa Bin Laden na Mr Simon umefanya ngoma ya ‘Baba Jeni’ kuwa bora sana. Kwenye wimbo huu, Maua Sama anatoa ya moyoni kuhusu mpenzi wake wa zamani kwa kusema kuwa hamuhitaji tena kwenye maisha yake.

https://www.youtube.com/watch?v=RLWv3vSoXyU

Party - Nandy ft Billnass & Mr Eazi

Kwenye ngoma ya ‘Party’, Nandy anajipa kazi ya kuwapeleka watu kwenye club na sehemu za mbalimbali starehe kupitia ngoma hii.  Nandy anawahasa watu kujiachia na kwenda kustarehe kwani maisha ni mafupi. Hii ni ngoma ambayo inawakutanisha kwa mara nyingine Nandy na Billnass pamoja na Mr Eazi ambaye ni msanii kutokea nchini Nigeria.

Acha Niongee - Nay Wa Mitego

Gwiji wa Hip-hop kutokea Tanzania Nay Wa Mitego amerudi tena na ngoma yake mpya ya kuitwa ‘Acha Niongee’ ambayo ndani yake ameainisha changamoto ambazo amezipitia kwenye harakati zake za muziki.

Leave your comment