‘Sukari’ ya Zuchu Yaweka Rekodi Mpya YouTube Tanzania

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Zuchu ameweka rekodi mpya kwenye muziki wake kupitia video ya ngoma yake ya ‘Sukari’ ambayo iliingia sokoni mwezi Januari mwaka wa 2021.

Kwenye mtandao wa YouTube, video ya ‘Sukari’ imeshatazamwa mara Milioni 60 mpaka sasa na hivyo kumfanya Zuchu kuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kuwa na video iliyotazamwa zaidi kwenye mtandao huo bila kumshirikisha msanii yeyote.

Soma Pia: Mbosso ‘For Your Love’, Ibraah ‘Addiction’ na Nyimbo Zingine Zinazovuma YouTube Tanzania Wiki Hii

Rekodi hiyo awali ilikuwa inashikiliwa na mwanamuziki Diamond Platnumz kupitia ngoma yake ya ‘Jeje’ ambayo Diamond amefanya mwenyewe bila kumshirikisha msanii yeyote. Mpaka sasa, video ya ‘Jeje’ imeshatazamwa mara Milioni 59 kwenye mtandao wa YouTube.

Kusherehekea rekodi hiyo mpya kwenye muziki wake, Zuchu kupitia akaunti ya Instagram ameandika "Ikumbukwe tangia Tanzania ipate uhuru Zuchu ndo msanii pekee mwenye wimbo wenye views nyingi akiwa peke ake Alone bila collaboration ukifuatiwa na Jeje."

Soma Pia: Nandy Atoa Lawama Zake kwa Waandaaji wa Tuzo za AFRIMA

Aidha pia video hiyo ya ‘Sukari’ imeweka rekodi ya kuwa ngoma ya msanii wa kike iliyotazamwa zaidi barani Afrika kwa mwaka 2021 kwenye mtandao wa YouTube.

Kando na ‘Sukari’, video nyingine kutoka kwa Zuchu zilizotazamwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube ni pamoja na ‘Cheche’ ambayo kufikia sasa imetazamwa mara Milioni 26 pamoja na ‘Litawachoma’ ambayo imetazamwa mara Milioni 21. Kwenye ngoma zote mbili ameshirikiana na Diamond Platnumz.

https://www.youtube.com/watch?v=CCmItvVgn6Q

Leave your comment