Nandy Atoa Lawama Zake kwa Waandaaji wa Tuzo za AFRIMA

[Picha: The Citizen]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Nandy ameamua kutoa malalamiko yake kwa waandaaji wa tuzo za AFRIMA kutokana na waandaaji wa tuzo hizo kutowajali wasanii pindi wanapohudhuria tuzo hizo.

Akiongea kwenye mkutano aliofanya kwenye kituo cha EFM, Nandy alisema kuwa waandaaji wa tuzo hizo hawawapi wasanii hadhi na thamani wanayostahili na hivyo kupelekea wasanii wengi kutoshiriki kikakimilifu kwenye tuzo.

Soma Pia: Rayvanny Akerwa na Kukosa Kutajwa na Rais Kama Msanii Aliyeteuliwa Tuzo za AFRIMA

"Kiukweli ni sisi tu mashabiki tumeyabeba sana haya matuzo ya Nigeria au za nchi za nje kiasi cha kwamba yanakuja yanatuumiza sisi lakini tunayoyapata huko ni mengi, treatment ni mbaya so sorry for saying this. Treatment sio nzuri arrangement sio nzuri," aliongea Nandy kwa malalamiko makubwa.

Aidha, Nandy alizidi kudadavua kuwa alipata nafasi ya kukutana na Zuchu kwenye ndege kipindi wanarudi kutoka kwenye tuzo hizo na kama yeye, Zuchu pia hakuridhika na maandalizi ya tuzo hizo.

"Wakati narudi kutoka South Africa na yeye alikuwa anatoka Nigeria tukapanda ndege moja siti moja tumeizungumzia sana hii. Ye mwenyewe (Zuchu) alikuwa ananiambia anatamani kesho yake angetweet kwa makasiriko aliyokuwa nayo. Sema anahisi akisema wangesema we unaongea kwa sababu umekosa tuzo,"alizungumza Nandy.

Mwisho, Nandy alitumia fursa hiyo kuwahasa wadau mbalimbali wa sanaa na muziki nchini Tanzania kuandaa tuzo zao wenyewe ili kuweza kukidhi na kukuza soko la muziki nchini Tanzania badala ya kutegemea tuzo za nje.

Leave your comment