Rayvanny Akerwa na Kukosa Kutajwa na Rais Kama Msanii Aliyeteuliwa Tuzo za AFRIMA

[Picha: Kidevu]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki wa bongo Rayvanny ameelezea kukerwa na kisa cha jina lake kutokewepo kwenye orodha ya wasanii walioteuliwa kwenye tuzo za Afrima.

Orodha hiyo ilikabidhiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu ili awapongeze wasanii hao kwa uteuzi huo na kuiwakilisha vizuri Tanzania kwenye tasnia ya muziki.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Lava Lava Aachia ‘Ng’ari Ng’ari’

Japo Rayvanny alikuwa ametuiliwa katika vitengo kadhaa kwenye tuzo za Afrima, jina lake halikuwepo kwenye orodha hiyo ambayo ilisomwa na Rais Samia.

Hili lilimkera Rayvanny kiasi cha yeye kuandika ujumbe mrefu kwenye ukurasa wa Instagram akilalamikia kisa hicho.

"I was so dissapointed mimi ni mmoja wa washiriki katika Tuzo Media imepost washiriki wa afrima and my name was not there na wakati nipo kwenye tuzo na nina more than one category, na list va washiriki kapewa mh rais na kawapongeza na jina langu halipo imagine," chapisho la Rayvanny kwenye ukurasa wake wa Instagram lilisomeka.

Soma Pia: Diamond, Rayvannny, Harmonize na Wasanii Wengine Waliotazamwa Zaidi YouTube Tanzania Mwezi Novemba

Rayvanny aliwashauri wanahabari kutumia picha yake wakati wanaripoti kumhusu yeye au kisa chochote chenye jina lake.

 "Blogs. Kama kuna sehemu kuna habari yangu iwe charts zozote iwe habari inayonihusu au nipo kwenye top rank ya charts zozote au anything kindly use my picture. Coz huwa naona sehemu nyingi nipo kwenye top rank alafu picha yangu kwenye post haipo afu unakuja kutag tu jina langu kwenye caption seriously?" Aliandika Rayvanny.

Leave your comment