Diamond, Rayvannny, Harmonize na Wasanii Wengine Waliotazamwa Zaidi YouTube Tanzania Mwezi Novemba
1 December 2021
[Picha: The Standard]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Soko la muziki nchini Tanzania limezidi kukua na kunawiri na mwezi Novemba umezidi kudhihirisha hilo kwani wasanii tofauti tofauti kutokea Tanzania wamefanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube.
Wafuatao ni wasanii watano kutoka Tanzania ambao wamefanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube kwa mwezi Novemba:
Soma Pia: Alikiba Adhibitisha Tamasha Nchini Kenya Kupitia 'Only One King Tour'
Diamond Platnumz
Simba kutokea WCB Diamond Platnumz ameendelea kunguruma kwenye mbuga ya YouTube kwa mwezi Novemba baada ya kazi zote kutazamwa mara Milioni 29.4. Mwezi Novemba Diamond hakupakia video yoyote kwenye akaunti yake ya YouTube tangu alipoachia ‘Gimmie’ mwezi Oktoba.
Rayvanny
Chui kutokea Next Level Music Rayvanny ameshika nafasi ya pili kwa mwezi Novemba kwani kazi zake zote zimetazamwa mara Milioni 19.5. Kwa mwezi Novemba Rayvanny aliachia video ya ngoma yake ya ‘Baila’ ambayo kufikia sasa imetazamwa mara Milioni moja kwenye YouTube.
Harmonize
Teacher Harmonize ameendelea kufanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube kwani mwezi Novemba ametazamwa mara Milioni 18.7. Harmonize kufanya vizuri YouTube kumechagizwa haswa na albamu yake ya ‘High School’ ambayo ilitoka Novemba 5, pamoja na video ya ‘Outside’ ambayo ilitoka wiki mbili zilizopita.
Mbosso
King Khan anashika namba nne kwani kwa mwezi Novemba ametazamwa mara Milioni 13. 5. Hii imechagizwa hasa na ngoma yake ya ‘Your Love’ ambayo alimshirikisha Zuchu.
Zuchu
Malkia wa Bongo Fleva Zuchu amezidi kufanya vizuri Youtube kwani kwa mwezi Novemba ametazamwa mara Milioni 8.4. Ikumbukwe kuwa Zuchu hajatoa ngoma yoyote binafsi tangu aachie ‘Yalaaa’ mwezi Agosti mwaka huu.
Leave your comment