Alikiba Adhibitisha Tamasha Nchini Kenya Kupitia 'Only One King Tour'

[Picha: Africa Billboard]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mfalme wa muziki wa bongo Alikiba ametangaza rasmi kuwa atazuru mkoa wa Naivasha nchini Kenya kupitia ziara yake ya muziki iliyopewa jina la 'Only One King Tour'.

Alikiba kupitia chapisho lake mtandaoni alisema kuwa atatumbuiza katika hoteli ya Lake Naivasha Resort mnamo tarehe 11 mwezi Disemba.

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa na Ibraah, Nandy na Maua Sama Tanzania Wiki Hii

Aliwahimiza mashabaki wanunue tiketi ya tamasha hilo kwani litakuwa la kukata na shoka.

"Naivasha!! Naivasha!! Kenya, Season is here, Only One King Tour in Kenya!! I will be performing Live at Lake Naivasha Resort on 11th December 2021. Get Your tickets now it's going to be an epic experience. Usikose Mtu Wangu," Alikiba aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Ujumbe huu umewasisimua mashabiki wa Alikiba kutoka nchini Kenya kwani hii itakuwa fursa ya kipekee kumwona staa huyo akitumbuiza mbashara.

Soma Pia: Vanessa Mdee Awahisi Wasanii wa Tanzania Dhidi ya Kutumika Vibaya na Makampuni

Hapo awali Alikiba alitangaza ujio wa ziara yake ya muziki ambayo pia lengo lake kuu ni kuipigia kampeni albamu yake ya 'Only One King'. Alikiba alisema kuwa ziara hiyo vile vile ilitokana na mafanikio makubwa ambayo albamu yake ilikuwa imepata.

"One month after dropping Only One King Album, mapokezi yake yamekua makubwa sana!! Asanteni sana. And December is here, let’s get the party started, I’m officially announcing Only One King tour is on. Tunaanza na Rock City, Mwanza on 17th December!! Save The Date," ujumbe wa Alikiba ulisomeka.

Leave your comment