Vanessa Mdee Awahisi Wasanii wa Tanzania Dhidi ya Kutumika Vibaya na Makampuni
30 November 2021
[Picha: The Standard]
Mwandishi: Brian Sikulu
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Staa wa muziki wa bongo Vanessa Mdee amewatahadharisha wasanii dhidi ya kukubali kutumika vibaya na makampuni ambayo yanataka kuendeleza maslahi yao kwa kutumia umaarufu wa wasanii hao.
Kupitia ukurasa wake wa kijamii, Vanessa Mdee alisimulia jinsi benki moja maarufu ilikosa kumlipa hata baada ya yeye kutangazwa kuwa balozi wa benki hiyo.
Soma Pia: Wasifu wa Vanessa Mdee, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake
Vanessa Mdee, ambaye anajulikana kwa ngoma zake kali kama vile 'Niroge', alifichua kuwa japo benki aliyohudumia ilikuwa bora, kufikia sasa wamekimia na hawajatii makubaliano waliokuwa nayo ya malipo.
Kupitia chapisho aliloliweka mtandaoni, Mdee aliwashauri wasanii kuwa makini wanapofanya biashara na makampuni.
"Artists na watu maarufu Tanzania please don’t let these corporate companies take advantage of you. Mpaka leo lile benki halijamaliza kunilipa. Japo kiukweli ni benki bora but wameona wajikaushe. Yote kheri," Vanessa Mdee aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Soma Pia: Nyimbo 5 zake Vanessa Mdee Zilizovuma Bongo
Vanessa Mdee kabla ya kustaafu kwenye muziki mwaka jana, alifanya kazi na mashirika makubwa nchini Tanzania.
Ujumbe wa Mdee unatokea muda mfupi tu baada ya malkia wa muziki wa bongo Zuchu pia kulalamika kuhusu makampuni kutowalipa wasanii haswaa wale wa kike. Zuchu alichapisha ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram ambako alilalamika kuhusu kisa ambacho alikosa kulipwa.
Leave your comment