Nyimbo 5 zake Vanessa Mdee Zilizovuma Bongo

[Picha: IGA]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Kama unafuatilia muziki kutokea Tanzania basi bila shaka utakuwa unamfahamu Vanessa Mdee. Mwanadada mwenye sauti ya ndege, mnana ambaye alianzia kwenye utangazaji lakini ilipofika mwaka 2013, aliamua kugeuza shilingi na kuingia kwenye muziki baada ya kuachia wimbo wake wa ‘Closer’ ambao ulimtambulisha vyema.

Soma Pia: Wasifu wa Vanessa Mdee, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

Tangu aanze muziki miaka nane nyuma Vanessa ameshafanya kazi na wasanii wakubwa Afrika kama Reekado Banks, Mr P, KO, Distruction Boyz na wengineo na collabo hizo zimepelekea yeye kutambulika sana na kuzoa tuzo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania kama Afrimma pamoja na nyinginezo nyingi.

Kwa sasa yupo nchini Marekani akiwa yuko kwenye mapumziko ya kimuziki lakini sio vibaya kujikumbushia nyimbo zake tano ambazo zimefanya vizuri sana:

Juu ft Juma Jux

Juu ni wimbo wa mapenzi ambao Vanessa aliuachia Desemba 2016 na watanzania walipokea wimbo huu kwa mikono miwili. Ngoma hili lilithibitishwa kipindi Vanessa na Jux walipokuwa kwenye tamasha lao la pamoja la ‘In Love & Money Tour’ mwaka 2018 kwani wimbo huo ulikuwa unapagawisha mashabiki mara tu ulipokuwa unatumbuizwa na wanamuziki hao jukwaani. Kufikia sasa,video ya wimbo huu imeshatazamwa mara Milioni 4.4 kwenye mtandao wa YouTube.

Never Ever

Ilipofika mwaka 2015, Vanessa aliungana na mtayarishaji muziki Nahreel kufanya wimbo wa ‘Never Ever’. Wimbo huu ulithibitisha kuwa yeye ndio malkia wa muziki wa RnB hapa nchini Tanzania kutokana na namna ambavyo aliimba vizuri na kwa hisia mno. Kusindikiza ‘Never Ever’, Vanessa aliachia video ya wimbo huo iliyofanyika huko nchini South Afrika Johanesburg na kufikia sasa umeshatazamwa mara Milioni 3.5 kwenye mtandao wa YouTube.

 Wet ft Gnako

‘Wet’ ni makhususi kabisa kwa watu wanaopenda muziki wa kuchangamka. Kipindi wimbo huu ulipotoka ulichezwa sana kwenye clubs tofauti tofauti ndani na nje ya Tanzania. Ubunifu wa rapa Gnako aliyetawala kwenye kiitikio pamoja na mdundo wenye nguvu kutoka kwa Nahreel umefanya ‘Wet’ usiweze kuchuja kwenye masikio ya msikilizaji. Wimbo huu umeshatazamwa mara Milioni 4.4 kwenye mtandao wa YouTube.

Kisela ft Mr P.

‘Kisela’ ni wimbo ambao Vanessa Mdee anaimba kwa hisia sana. Alipokuwa anafanya mahojiano na Sky Walker miaka kadhaa nyuma, alikiri kuwa alikuwa analia wakati anarekodi wimbo huu kutokana na wimbo huu kubeba maana kubwa sana kwake. Ekelly kutokea Nigeria ndiye amehusika kuandaa wimbo huu huku Director Clarence alihusika kwenye video ya kazi hii ambayo kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 3 kwenye mtandao wa YouTube.

Thats For Me ft Distruction Boys & Prince Bulo

Ndani ya ‘Thats For Me’, Vanessa Mdee anajiachia na kuonesha ufundi wake kwenye kucheza dansi huku akisindikizwa na mdundo wa nguvu kutoka huko Afrika kusini. Kufikia sasa wimbo huo umetazamwa mara sabini na nane elfu kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=QI3SlwH_dXc

Leave your comment