Wasifu wa Vanessa Mdee, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

[Picha: Capital]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Vanessa ni nani na ana miaka mingapi?

Jina la usani: Vanessa Mdee

Jina Halisi: Vanessa Hau Mdee

Tarehe ya kuzaliwa: 16th July, 1988 (32 years old)

Aina ya muziki: RnB‎, ‎Afro pop‎, ‎Hip Hop‎ and Bongo Flava.

Thamani Yake: Anakisiwa kuwa na thamani ya dola milioni moja

Pata Ubashiri wa Mechi Katika ya Real Madrid na Chelsea 

Maisha ya mapema ya Vanessa yalikuwaje?

Vanessa Hau Mdee alizaliwa Arusha Tanzania ila maisha yake kwa wingi aliishi  mjini New York. Alisoma na kuhitimu kutoka shule ya upili ya Arusha. Kisha alihudhuria Chuo Kikuu cha Katoliki cha Afrika Mashariki  nchini Kenya alikosomea digrii ya Uanasheria.

Fungu la Leo Zaburi 118:14

Vanessa Mdee alianza  muziki  lini?

Vanessa alijitokeza kwenye tasnia ya muziki mwishoni mwa mwaka 2012. Alitoa wimbo wake wa kwanza 'Mimi na Wewe' baadaye mwaka huo akimshirikisha Ommy Dimpoz. Mwanzoni mwa mwaka 2013, aliachia wimbo wake binafsi wa kwanza 'Closer' ambao ulimpa umaarufu mkubwa  nchini Tanzania na hata ikampa tuzo nne maarufu mwaka huo katika tasnia ya muziki wa Tanzania.

Soma Pia: Wasifu wa Nandy, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

Tokea hapo Vanessa aliendelea kupata umaarufu kupitia mziki wake. Amefanya pia kazi na wasanii anuwai wakubwa  barani Afrika ikiwa ni pamoja na; Reekado Banks, Navio, Orezi, Jux, Gnako, Ice Prince, Sauti Sol, Rayvanny kati ya wengine wengi. Mnamo 2018, alitoa albamu yake ya kwanza 'Money Monday' ambayo ina nyimbo 18.

 Tuzo na Uteuzi wa Vanessa Mdee

  • Tuzo 5 za Muziki Tanzania
  • All Africa Music Awards  (Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki).
  • African Muzik Magazine Awards (Msanii bora wa Kike Afrika Mashariki)
  • All Africa Music Awards (Pop Bora ya Afrika)
  • 2 Abryanz Style and Fashion Awards (Msanii wa Kike Mtindo zaidi Afrika Mashariki)
  • Africa Entertainment Awards (Msanii Bora wa Kike Afrika)

Vanessa Mdee ana mahusiano na nani?

Vanessa Mdee kwa sasa anachumbiana na muigizaji na mwanamuziki wa Amerika Rotimi. Wawili hao walianza kuchumbiana baada ya Mdee kuachana na mwanamziki mwenzake Juma Jux mwaka 2019. Hivyo Vanessa kwa sasa anaishi na mchumba wake Rotimi aliyempa pete ya kuchumbiana mwezi Januari 2021.

Kwa nini Vanessa Mdee aliacha muziki?

Mwaka jana, Vanessa Mdee aliwashanagaza mashabiki alipotangaza kwamba anaacha muziki. Msanii huyo mwenye umri wa miaka 32 alibaini kuwa ameamua kuacha muziki ili kuzingatia mambo mengine kama kuwa mtetezi wa uaminifu, urembo na kukabiliana na msongo wa akili. Mwimbaji huyo wa 'Cash Madame' alisema tasnia ya muziki ni ya Ushetani, na kwa hivyo ni kikwazo kwa dhamira yake mpya maishani.

Leave your comment