Nyimbo Mpya: Lava Lava Aachia ‘Ng’ari Ng’ari’

[Picha:  Lavalava Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Bongo Lava Lava ameachia wimbo mpya wenye jina ‘Ng’ari Ng’ari’.

Kwenye ngoma hii, Lava lava anatumia kipawa cha sauti yake kuonesha namna ambavyo amezama kwenye penzi jipya pamoja na kutuma ujumbe kwa mpenzi wake wa zamani kuwa hamuhitaji tena.

Kwenye aya ya kwanza ya ngoma hii Lava lava anaimba "Nimetulizana ndege kwa kiota sitoki mambo mwororo. Nimenasiana hata kwa kukokotwa sing'oki. Nishasahau zamani kushikana mashati mizozo mapenzi gani kila kukicha vibonzo."

Ngoma hii ni muendelezo wa Lava lava kuonesha uwezo wake wa kuandika nyimbo za mapenzi. Ngoma hii imepikwa na watayarishaji wawili wa muziki kutokea Tanzania ambao ni Lizer Classic kutokea Wasafi Records pamoja na Gopabeatz ambaye pia alihusika kutayarisha ngoma ya "Inatosha" ya kwake Lava lava.

Kabla ya kuachia ngoma hii Lava lava alikuwa anatamba na ngoma yake iliyonakshiwa na vionjo vya zilipendwa ya kuitwa ‘Inatosha’ ambayo iliingia sokoni Oktoba 23 mwaka huu.

Kabla ya hapo, msanii huyo kutokea WCB alikuwa anatamba na ‘Itetemeshe’ aliyofanya na Bob Junior. Mwaka huu umekuwa ni mwaka wa baraka sana kwa Lavalava kwani msanii huyo ameweza kuachia miradi tofauti tofauti ya kimuziki ambayo imetikisa Tanzania ikiwemo EP yake ya ‘Promise’ iliyotoka miezi tisa iliyopita.

https://youtu.be/gK5KjpqRTDE

Leave your comment