Alikiba Atangaza Ujio wa ‘Only One King’ Tour

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki wa bongo Alikiba ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa lebo ya King's Music ametangaza ujio wa ziara yake ya muziki nchini Tanzania.

Ziara hiyo liyopewa jina la 'Only One King Tour' kutokana na jina la albamu yake ya hivi karibuni inatarajiwa kuanza mnamo tarehe 17 mwezi Disemba katika ukumbi wa Rock City, mjini Mwanza.

Soma Pia: Yogo Beats Asimulia Changamoto Alizopitia Akianda Albamu yake Alikiba 'Only One King'

Katika ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa kijamii, Alikiba alieleza kuwa ziara hiyo inatokana na mafanikio makubwa ambayo albamu yake ya 'Only One King', iliyotoka mnamo tarehe 7 mwezi wa Oktoba, imepata.

"One month after dropping Only One King album, mapokezi yake yamekua makubwa sana!! Asanteni sana. And December is here, let’s get the party started, I’m officially announcing Only One King tour is on. Tunaanza na Rock City, Mwanza on 17th December!! Save The Date. For bookings/sponsorship etc wasiliana na management yangu @kingsmusicrecords kupitia emailalikiba@gmail.com," chapisho la Alikiba mtandaoni lilisomeka.

Soma Pia: Alikiba Afichua Sababu ya Kuita Albamu Yake ‘Only One King’

Albamu hiyo ambayo ilikuwa na jumla ya nyimbo kumi na sita iliwaleta pamoja wasanii tajika kutoka sehemu tofauti za bara la Afrika. Baadhi ya wasanii wakubwa waliohusishwa mle ndani ni pamoja na Rude Boy, Patoranking, Khaligraph, Mayorkun na wengine wengi.

Kufikia sasa, baadhi ya ngoma ambazo zimefanya vizuri mno kwenye mtandao wa YouTube kutoka kwenye albamu hiyo ni pamoja na 'Songi Songi remix' (takriban watazamaji milioni moja), 'Bwana Mdogo'(takriban watazamaji milioni mbili nukta tatu), 'Oya Oya' (tarkiban watazamaji milioni tatu nukta tatu), 'Salute' (takriban watazamaji milioni tano nukta tisa), 'Jealous' (takriban watazamaji milioni nane nukta saba) na nyinginezo nyingi.

Leave your comment