Yogo Beats Asimulia Changamoto Alizopitia Akianda Albamu yake Alikiba 'Only One King'
18 November 2021
[Picha: Opera News]
Mwandishi: Brian Sikulu
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Mtayarashaji wa muziki kutoka Tanzania Producer Yogo Beats amefunguka kuhusu changamoto alizopitia katika utayarishaji wa albamu ya Alikiba ya 'Only One KIng'.
Jambo moja ambalo limekua la kipekee kwa albamu hiyo ni kuwa nyimbo zote kumi na sita zilizomo humo ndani zimetayarishwa na producer mmoja ambeye ni Yogo.
Soma Pia: Rayvanny Adokeza Ujio wa Wimbo Mpya na Maluma Baada ya Kuachia ‘Mama Tetema’
Kupitia mahojiano ya hivi karibuni, Producer Yogo alisema kuwa haikuwa kazi rahisi kutengeneza nyimbo zote katika albamu hiyo na kuna changamoto mingi ambayo alipitia.
Albamu hiyo ambayo ilichukua muda wa mwaka mmoja kutengenezwa iliwahusisha wasanii tofauti kutoka bara la Afrika.
Soma Pia: Professor Jay Adai Wasanii wa Bongo Wana Upungufu kwenye Ustadi wa Kutunga Nyimbo
Changamoto kubwa ambayo Yogo alikumbana nayo kwenye safari ya utengenezaji wa albamu hiyo ilikuwa ugomvi wa kitaaluma na Alikiba.
Producer Yogo alisema kuwa mgongano wa mawazo baina yake na Alikiba ndio iliyokuwa chanzo cha ugomvi mwingi ila mwisho wa siku walikubaliana.
Aliongezea kuwa tofauti na utayarishaji wa ngoma moja, utayarishaji wa albamu ni mradi ambao unahitaji uwekezaji wa akili na muda mwingi sana. Tofauti na jinsi watu wengi wanavyojua, albamu hiyo ilikuwa na zaidi ya nyimbo 16 ila mwisho wa siku baada ya kuchongwa ndio zikasalia kumi na sita.
"Unajua albamu sio nyimbo. Album ni project ambayo inakulazimu utumie akili. Utumie busara na hekima yako kuifanya, kwa sababu kutengeneza nyimbo kumi na sita, sio ati ni nyimbo kumi na sita tu. ni nyimbo ambazo huenda zikawa zaidi ya kumi na sita mara tatu ambazo zimekusanywa zikapatikana kumi na sita. Kwa hivyo kutengeneza izo nyimbo zote na binadamu ambaye hamjawahi kukaa sehemu moja, hamjawahi kuzaliwa tumbo moja, hamjawahi kuishi nyumba moja, hamna experience yoyote labda mlicheza pamoja ni kitu kikubwa sana. Ujue kuna vingi vilitokea hapo, kuna ubishani, ugomvi vingi tu yaani," Producer Yogo alieleza.
Leave your comment