Professor Jay Adai Wasanii wa Bongo Wana Upungufu kwenye Ustadi wa Kutunga Nyimbo

[Picha: Professor Jay Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii mwenye heshima kubwa kwenye tasnia ya muziki wa Tanzania Professor Jay amedai kuwa kuna upungufu wa ustadi wa kutunga nyimbo miongoni mwa wanamuziki wa kizazi kipya.

 Kwa mujibu wa rapa huyo, wasanii wa sasa wamekuwa wavivu na hawawekezi katika ubora wa muziki haswaa kwenye maudhui.

Soma Pia: Professor Jay Asimulia Sababu ya Diamond Kulia Alipofanya Kazi na Yeye

Alieleza kuwa wasanii wengi wako na haraka ya kupata mafanikio na kutoa nyimbo na hivyo basi hawazingatii ujumbe uliomo kwenye ngoma.

Akilinganisha usanii katika kizazi cha sasa na kile cha zamani, Jay alisema kuwa wasanii wa kale walikuwa wakitumia muda mwingi na maarifa katika kutunga nyimbo zao.

Wasanii wa zamani, kulingana na Professo Jay, walitumia ngoma zao kutuma ujumbe mzito kwenye jamii. Nyimbo za wasanii hao zilikuwa zenye heshima na hata zingeweza kusikilizwa na watu wa umri wote.

Hali hii hata hivyo imebadilika kwenye muziki wa kizazi kipya kwani baadhi ya ngoma haziwezisikilizwa na watu wa umri wote.

Soma Pia: Professor Jay Afichua Sababu ya Uhasama Baina ya Wasanii wa Kizazi Kipya na Cha Kale 

"Sasa hivi tumekuwa wavivu tu yaani tunataka hela bila kufanya kazi. Kwa kifupi wasanii wa sasa wengi wanataka kukaba kupitia uongo wa sanaa. Yaani wanataka kufanya kitu wapate maslahi wapate pesa bila kuimba kitu cha maana, na bila kuwekeza katika kizazi kinachofuata. Ina maana kwamba wenyewe wakimaliza na wakiisha kwenye hii game, yaani sanaa iwe tupu tu wasiache urithi kwa kizazi kingine," Professor Jay ambaye amekuwa kwenye muziki kwa muda mrefu alieleza.

Leave your comment