Professor Jay Afichua Sababu ya Uhasama Baina ya Wasanii wa Kizazi Kipya na Cha Kale

[Picha: CitiMuzik]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki maarufu Professor Jay amedai kuwa kuna uhasama mkubwa baina ya wanamuziki wa kizazi kipya na wale wa kizazi cha kale. Rapa huyo ambaye amekuwepo kwenye tasnia ya muziki wa Tanzania kwa muda mrefu sana, alieleza kisa cha uhasama huo na athari zake kwenye muziki.

Professor Jay alikuwa akizungumza katika mahojiano na Wasafi TV aliposimulia jinsi baadhi ya wasanii ambao walivuma enzi za zamani wamepuuzwa na kizazi kipya.

Soma Pia: Professor Jay Asimulia Sababu ya Diamond Kulia Alipofanya Kazi na Yeye

Kwa mujibu wa rapa huyo, wasanii waliounda msingi wa muziki wa Tanzania kupuuzwa, huku wale wa kizazi kipya kusheherekewa ndio sababu kuu ya uhasama baina ya makundi haya mawili.

Professor Jay aliongezea kuwa yeye binafsi kama msanii hujitahidi kuziba pengo lililopo baina ya wasanii wa bongo wa kale na wa kizazi kipya. Alisema kuwa hii ndio njia pekee ya kuhakikisha kuwa nyota ya wasanii wa zamani inaendelea kung'aa.

Alitoa mfano wa jinsi alivyofanya kazi na wasanii ambao wanavuma kwa sasa ikiwemo Diamond Platnumz, Young Lunya, Maua Sama na wengine wengi.

"Ili tufanikishe huu muziki ufike kwenye level ya juu lazima tuwe na chemistry na ushirikiano kati ya wasanii wa sasa na wa zamani. Wale wa zamani wana heshima yao, of course wasanii wa sasa wengi hawaheshimu wasanii wa zamani. Lakini wa zamani pia wana bifu yao wakiona msanii anafanikiwa na anapata mipunga sasa hivi, kunakuwa na kama vitu fulani haviendelei," Professor Jay alieleza.

Leave your comment