Professor Jay Asimulia Sababu ya Diamond Kulia Alipofanya Kazi na Yeye

[Picha: Ghafla]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Moja kati ya nyimbo ambazo zilimwongezea mwanamuziki nyota Diamond Platnumz umaarufu kwenye tasnia ya muziki ni wimbo wa 'Kipi Sijaskia' ambayo alishirikishwa na msanii wa mtindo wa Hip-Hop Professor Jay.

Ngoma hiyo iliyotoka mwaka wa 2014 ilivuma sana na kufikia sasa imetazamwa zaidi ya mara milioni saba kwenye mtandao wa YouTube.

Soma Pia: Professor Jay Afichua Sababu ya Uhasama Baina ya Wasanii wa Kizazi Kipya na Cha Kale

Wasichokijua wengi ni hadithi iliyopo nyuma ya ngoma hiyo na jinsi mistari ya ngoma hiyo zilimmaliza Diamond Platnumz wakati wakiurekodi.

Professor Jay amesimulia jinsi ngoma hiyo ilivyotengenezwa kuanzia 'audio' hadi video yake. Suala moja ambalo alilizungumzia kwa kina ni jinsi Diamond alipandwa na hisia wakati wa kurekodi nyimbo hiyo, jambo ambalo lilichangia katika kuongeza ubora wake.

Jay alisema kuwa Diamond aliguswa mno na mistari ya ngoma hiyo kwani mambo mengi yaliyotajwa mle ndani ni yale ambayo alikuwa akipitia kwenye tasnia ya muziki. Jambo hili lilimfanya kulia wakati wa kurekodi wimbo huo na hisia zake zikaongeza uhalisia wa ngoma ya 'Kipi Sijaskia'.

Soma Pia: Harmonize Akataa Kulinganishwa na Msanii Yeyote, Aapa Kuibadilisha Tasnia ya Muziki

"Kwanza pamoja na kumtafuta Diamond, lakini yeye wakati anarekodi humo studio alikuwa anarekodi wakati analia. Alikuwa na feeling ya hali ya juu sana, sisi tumekaa hapo, tumemwacha yeye booth tupo pembeni, jamaa anarekodi na yuko na feeling ya hali ya juu. Tukawa tunaulizana na Majani, huyu jamaa analia nini mzee?" Professor Jay alisema.

"Tukaja kugundua baadaye yeye alituambia kwanza yale mambo ambayo yalikuwa yakizungumzwa mule, either amepitia ama yalikuwa yamemzunguka kwa kipindi kile," Jay aliongezea.

Leave your comment