Rayvanny Adokeza Ujio wa Wimbo Mpya na Maluma Baada ya Kuachia ‘Mama Tetema’

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Nyota ya msanii Rayvanny inazidi kung'aa kimataifa baada ya yeye kudokeza ujio wa kazi yake mpya ambayo inaonekana kuwa kolabo na staa wa muziki wa Kolombia Maluma.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rayvanny alichapisha kipande cha video ambayo ilimwonyesha akiwa studio wakati wa kurekodi wimbo huo.

Soma Pia: Mtv Base Wampongeza Rayvanny Baada ya Kutumbuiza Kwenye MTV EMA

Kwenye ngoma hii mpya Rayvanny amefanya kitu kipya na tofauti sana, kitu ambacho kwa kiasi fulani hakikutarajiwa.

Chui, kama anavyofahamika kiutani, ameimba kwa lugha ya Kihispania. Msanii huyo amefahamika zaidi kwa kuimba kwa lugha ya Kiswahili na wakati mwingine Kingereza.

Hili ni jambo kubwa sana kwa staa huyo ambaye hivi karibuni amegonga vichwa vya habari kutokana na mafanikio yake, kwani lugha hii ya kigeni itamsaidia kupanua soko lake la muziki kimataifa.

Soma Pia: Serikali ya Tanzania Yampongeza Rayvanny Kwa Kuandikisha Historia Kwenye Tuzo za MTV EMA

Kwenye kipande hicho cha wimbo, Rayvanny anasikika akiimba kwa sauti ya kumtoa nyoka pangoni na melody za kutuliza na kupendaza mno.

Vile vile alimtag msanii Maluma kwenye video hiyo kuashiria kuwa huenda ikawa kolabo nyingine baada ya wawili hao kutoa 'Mama Tetema' ambayo imevuma mno kimataifa.

Ikimbukwe kuwa ni kupitia ngoma ya 'Mama Tetema', ambayo ni remix ya wimbo asili wa Rayvanny 'Tetema, ndio Rayvanny aliweza kuandikisha historia ya kuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika kutumbuiza kwenye tuzo za MTV EMA.

Rayvanny amepongezwa mno na wadau mbali mbali kwenye tasnia ya muziki wa Tanzania kutokana mafanikio yake ya kimataifa.

Leave your comment