Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Mtv Base Wampongeza Rayvanny Baada ya Kutumbuiza Kwenye MTV EMA
16 November 2021

[Picha: Gazeti App]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Kituo cha muziki kikubwa kutoka Afrika Kusini MTV Base kimempa hongera Rayvanny kufuatia yeye kutumbuiza kwenye tuzo za MTV EMA.
Kupitia ukurasa wa Instagram, MTB Vase ilichapisha picha inayomuonesha Rayvanny akiwa na Maluma na kisha kumpongeza msanii huyo kwa kutumbuiza vizuri kwenye tuzo hizo.
Soma Pia: Serikali ya Tanzania Yampongeza Rayvanny Kwa Kuandikisha Historia Kwenye Tuzo za MTV EMA
Kituo hicho pia na kimeahidi kuzidi kuunga mkono muziki wa Afrika uzidi kwenda duniani.
"Moja kati ya onesho bora sana jana usiku kwenye tuzo za EMAs kutoka kwa Rayvanny akiwa jukwaani na msanii kutokea Latin Maluma katika uzinduzi wa kipekee kabisa wa wimbo wao ‘Mama Tetema’. Tuna shauku kubwa sana kuhusu kesho ya muziki wa Afrika na tutaendelea kutoa nafasi ili kuonesha vipaji na utamaduni kutokea Africa," lilisomeka chapisho ambalo lilikuwa kwa lugha ya kiingereza.
Pongezi hizo kutoka MTV Base zinakuja siku mbili baada ya Rayvanny kutumbuiza kwenye tuzo hizo ambazo zilifanyika huko nchini Hungary.
Soma Pia: Rayvanny Aweka Rekodi Baada ya Kutumbuiza Kwenye Tuzo za MTV EMA
Kutokana na onesho hilo, Rayvanny aliweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kutokea Afrika kutumbuiza kwenye tuzo hizo. Kwingineko, wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo kupitia mitandao ya kijamii ilitoa waraka kumpongeza Rayvanny kwa kuweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika kutumbuiza kwenye tuzo hizo.
Wasanii wengine kama Diamond Platnumz, Jux, G Nako, Shetta na Maua Sama pia walitoa pongezi kwa Rayvanny kwa hatua hiyo.
Weekly Top 10 songs

Trust No One3:13
chile-one-so-lucky4:02
Kamwambie3:47
Joy Is Coming3:08
Buwooma2:44
Udede Ft Msomali x Malume & Samas Alifata Hela Remix6:34
Msaliti 11:25
Leo3:39
Maringo4:00
NANI ft. Kamanda Pedeshee3:56
Top stories
- The Marathon
25 April
- Who Is Bad Beric
24 April
- Cashout by monyzoh boy
24 April


Leave your comment