Rayvanny Aweka Rekodi Baada ya Kutumbuiza Kwenye Tuzo za MTV EMA

[Picha: Pulse Live]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Rayvanny ameweka rekodi mpya kwenye muziki baada ya kutumbuiza kwenye tuzo za MTV EMA ambazo zilifanyika huko Hungary kwenye mji wa Budapest.

Rayvanny aliimba wimbo wa ‘Mama Tetema’ akiwa pamoja na msanii kutokea Columbia anayeitwa Maluma, na hivyo basi Rayvanny kuweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kutokea barani Afrika kutumbuiza kwenye jukwaa la tuzo hizo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Maluma Amshirikisha Rayvanny Kwenye ‘Mama Tetema’

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Rayvanny aliweza kumshukuru Maluma na timu yake kwa kumuwezesha kutumbuiza kwenye tuzo hizo na aliongeza kuwa hatua hiyo imepelekea muziki wa Tanzania kwenda kimataifa.

"I'm so honored to be the first African artist to perform at Mtv EMA. Big thanks to my brother Maluma and the whole team king lua vision clarapablo, New Chui Global way Africa, East Africa Tanzania to the world. Mama Tetema" aliandika Rayvanny kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Wadau tofauti tofauti wa sanaa nchini Tanzania ikiwemo watangazaji kama Fredrick Bundala na Mamy Baby walimpongeza Rayvanny kwa hatua hiyo huku wanamuziki pia kama Jux, Shetta, Maua Sama, G Nako na Shilole wote wakimpongeza msanii huyo kwa hatua hiyo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia Video ya Ngoma Yake Mpya ‘Outside’

Rayvanny tangu aanze muziki amekuwa ni msanii ambaye mara nyingi anaweka rekodi mbalimbali ikiwemo mwaka 2017 kuwa msanii wa kwanza kutokea Tanzania kupata tuzo ya BET.

Leave your comment