Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia Video ya Ngoma Yake Mpya ‘Outside’

[Picha: Tuko]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuzika tajika kutoka Tanzania Harmonize ameachia video ya ngoma yake mpya ‘Outside’.

‘Outside’ ni mojawapo ya wimbo kwenye albamu yake mpya ‘High School’.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Linex Aachia EP Mpya ‘Tatu za Mjeda’

‘Outside’ ni ngoma ambayo Harmonize anaongelea maisha yake zaidi na namna ambavyo kwa sasa anaishi maisha mazuri kutokana na kupambana sana.

Hii ni ngoma ambayo Harmonize anaonesha kuwa sasa ni muda wake wa kurahani maisha yake.

"Ooh yeah am not crazy from the middle…Yeah hustle every day I never sleep sleep coz outside When am falling I’m in loveIi go deep deep coz am outside" anaimba Harmonize kwenye aya ya kwanza.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Maluma Amshirikisha Rayvanny Kwenye ‘Mama Tetema’

Video ya ‘Outside’ pia imekoleza zaidi ujumbe wa wimbo huu ambapo Harmonize anaonekana akiwa amezungukwa na warembo wanaenda kustarehe.

Kwenye sehemu ya pili ya video, Harmonize anaonekana akiwa amevaa suti maridadi kabisa ambayo inaonesha kweli yeye ana pesa.

TG Omori kutokea Nigeria ndiye amehusika kuandaa video hii ambayo ina ubora wa picha wa kiwango cha kimataifa.

Kwa sasa watanzania wanasubiri kwa hamu video nyingine kutoka kwenye album ya ‘High School’ ya Harmonize.

https://www.youtube.com/watch?v=TW3lmdLTzjE

Leave your comment