Nyimbo Mpya: Maluma Amshirikisha Rayvanny Kwenye ‘Mama Tetema’

[Picha: Rayvanny Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota kutoka Columbia Maluma ameachia ngoma mpya kwa jina la ‘Mama Tetema’ akimshirikisha staa wa muziki wa bongo Rayvanny.

‘Mama Tetema’ ni remix ya wimbo wa Rayvanny ‘Tetema’ ambao aliutoa kwa ushirikiano na msanii nyota Diamond Platnumz.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia Video ya Ngoma Yake Mpya ‘Outside’

Wimbo asili wa ‘Tetema’ ulivuma sana mtandaoni na kupata mamilioni ya watazamaji, kufikia sasa takriban miaka miwili baada ya kutoka, ngoma hiyo imefikisha takriban watazamaji milioni sitini.

‘Mama Tetema’ kama vile ngoma asili ni ngoma ya kujiburudisha na ya kucheza. Wasanii hao kupitia ngoma hiyo wanawashawishi watu kunengua viuno na kusakata densi.

"Tipwa tipwa tetema (Oooh mama tetema). Haya twende tetema (Oooh mama tetema). Shuka chini tetema (Oooh mama tetema). Haya twende tetema (Oooh mama tetema). Tipwa tipwa tetema (Oooh mama tetema). Haya twende tetema (Oooh mama tetema). Shuka chini tetema (Oooh mama tetema)," Kipande cha mistari ya wimbo huo kinasomeka.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Video ya Ngoma Yake ‘Baila’

Maluma kwenye wimbo huu anaimba kwa lugha ya Kikolombia, na anaonekana kuchukua nafasi ambayo kwenye wimbo asili ilikuwa imechukuliwa na Diamond Platnumz.

Utayarishaji wa ngoma hii umesimamiwa na S2kizzy kutoka lebo ya WCB. Video kwa upande mwingine imeelekezwa na Jessy Terrero.

Video hiyo imerekodiwa katika mandhari yanayoonekana kuwa ya Kolombia. Ngoma hiyo ambayo ilichapishwa kwenye akaunti ya YouTube ya Maluma imepokelewa vizuri na mashabiki na tayari ishapata zaidi ya watazamaji laki moja chini ya saa moja.

https://www.youtube.com/watch?v=zOhDt1kin5o

Leave your comment