Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Video ya Ngoma Yake ‘Baila’
9 November 2021

[Picha: YouTube]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Bosi wa lebo ya Next Level Music Rayvanny ameachia video ya ngoma yake pendwa na inayofanya vizuri sana kwa sasa ‘Baila’.
‘Baila’ ni ngoma ambayo inapatikana kwenye EP yake aliyoiachia hivi karibuni inayoitwa ‘New Chui’ na hii ni video ya kwanza kabisa kuachiwa kutoka kwenye EP hiyo yenye nyimbo sita.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Maud Elka na Alikiba Waachia ‘Songi Songi’ Remix [Video]
‘Baila’ ni neno la kihispaniola lenye maana ya kucheza, na kwenye video ya ngoma hii, Rayvanny hajacheza mbali na maana ya neno hilo, kwani mwanzo hadi mwisho video hii imejaa mitindo ya tofauti tofauti ya dansi kutoka kwenye nchi mbalimbali za Amerika ya Kusini.
Kilichovutia zaidi kwenye video hii ni namna ambavyo Rayvanny alivaa mavazi yenye asili ya nchi za Columbia au Mexico kitu ambacho kimependezesha sana.
Video hii imeongozwa na Director Hanscana kutokea Tanzania ambaye pia alishafanya kazi na Rayvanny kwenye video ya ‘Lala’ ambayo Rayvanny alishirikiana na Jux.
Hii ni video ya kumi na moja kwa mwaka huu kutoka kwa Rayvanny. Kufikia sasa ameshatoa video tofauti tofauti kama ‘Kiuno’, ‘Lala’, ‘Sweet’, ‘Wanaweweseka’ na nyinginezo nyingi.
Weekly Top 10 songs

omelette4:28
Kyuma Radio and weasel ft Spice Diana4:07
ONLY YOU JESUS5:44
Kupenda nishapenda zaani3:12
CHAMPION GAL3:00
Nigina2:27
KIDUCHU2:12
Wano Wano2:15
Zabike2:50
Melody Ft Tunche the best3:20
Top stories
- Holy Boy (holyb374)
23 July
- Get New Hit Songs From Mock
23 July
- PLS GUYS SUPPORT ME
24 July


Leave your comment