Nyimbo Mpya: Maud Elka na Alikiba Waachia ‘Songi Songi’ Remix [Video]

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki Maud Elka ameachia video ya wimbo wake wa ‘Songi Songi’ Remix ambao amemshirikisha mwamba kutokea Tanzania Alikiba.

Wimbo wa ‘Songi Songi’ remix uliachiwa Agosti 20 mwaka huu na tangu kuachiwa kwake, mashabiki wengi wamekuwa na hamu ya kuona video ya ngoma hiyo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Alikiba Aachia Video ya ‘Bwana Mdogo’ Akimshirikisha Patoranking

Video ya ngoma hii imefanyika ufukweni na inamuonesha Alikiba na Maud Elka wakila raha na kufurahi kwenye fukwe kwa kufanya shughuli mbalimbali kama kuendesha pikipiki, kula chakula pamoja na shughuli nyingine ambazo wapendanao hufanya pamoja.

Aidha, ubunifu mkubwa umetumika katika kuandaa video hii ambayo kuanzia mandhari, mavazi na hata ubora wa picha ni wa kiwango cha juu sana.

Director Ivan kutokea Tanzania ndiye amehusika kuandaa video hii. Kando na video hii, pia amehusika kutengeneza video mbalimbali kama ‘Teacher’ ya Harmonize, ‘Tucheze’ ya Abby Chams, ‘Wow’ ya Marioo pamoja na ‘Fimbo’ ya Young Lunya.

https://www.youtube.com/watch?v=e046esyQcyM

Leave your comment