Nyimbo Mpya: Alikiba Aachia Video ya ‘Bwana Mdogo’ Akimshirikisha Patoranking
1 November 2021
[Picha: Alikiba Instagram]
Mwandishi: Brian Sikulu
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Mwanamuziki Alikiba ameachia video ya wimbo wake mpya ’Bwana Mdogo’ kutoka kwa albamu ya ‘Only One King’.
Alikiba amemshirikisha staa wa muziki kutoka Nigeria Patoranking kwenye ngoma hiyo mpya.
Wasanii hao wawili kwenye wimbo huu wanawasifu wachumba wao kwa sifa nzuri walizonazo. Alikiba ndiye anachukua mistari ya kwanza na kupitia sauti yake mwanana, anaimba jinsi mpenzi wake amejaliwa urembo na furaha anayopata kwenye mahusiano yao.
"My gal we ni matata, body matata mbaya eeh, Bwana mdogo umenikamata, unanicheza kama karata, Tulikutana kule Cape Cape town, Mpaka Accra Town dowtown, eeh, Eti una sifa za kudanga, Na mengi wanasema sijaona, Wivu umewaingia, Mungu kanionyesha ishara, Ndege wanashangilia na nitakupeleka ulaya, Wivu umewaingia, Mungu kanionyesha ishara, Ndege wanashangilia na nitakupeleka ulaya," Alikiba anaimba sehemu yake ya kwanza.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Lava Lava 'Inatosha', Maua Sama 'Zai' na Ngoma Zingine Zinazovuma Bongo Wiki Hii
Patoranking anaingia katika sehemu ya pili na pia kuachia mistari yake ya kumsifu mpenzi wake. Patoranking anaimba kwa lugha ya kingereza ambayo inazungumzwa sana nyumbani kwao Nigeria.
Mdundo wa ‘Bwana Mdogo’ umetengenezwa na mtayarishaji wa muziki Yogo Beats, ambaye pia ndiye amehusika katika kuziandaa ngoma zote kwenye albamu ya Alikiba, chini ya usimamizi wa lebo ya Kings Music.
Kampuni ya Ziiki media pia imehusika katika utayarishaji wa ngoma hii. Video imeelekezwa na Kyle White. Video hiyo imerokidiwa katika visiwa vya Zanzibar na inaonyesha mandhari mazuri ya sehemu hiyo.
‘Bwana Mdogo’ imepokelewa vizuri na mashabiki na ilikuwa ishatazanwa takriban zaidi ya mara nusu milioni wakati wa uchapisho wa nakala hii.
Leave your comment